| Gari lenye namba za usajili T 301 AKX linalosadaiwa kusababisha ajali katika barabara ya Kihesa - Chuo Kikuu cha Iringa kwenye maeneo ya Mtaa wa Ngome Kata ya Kihesa katika Manispaa ya Iringa. |
| Gari linalodaiwa kuwa lilikuwa katika mwendo kasi na kugonga gari lililokuwa likiingia barabarani. |
Watu watano wamenusurika kifo
baada ya magari walioyokuwa wakisafiria kugongana huku magari hayo yakihribika
vibaya.
Ajali hiyo iliyohusisha magari
madogo yenye namba za usajili T 301 AKX na T 434 CEL ilitokea jana usiku majira
ya saa moja usiku katika barabara ya Kihesa – Chuo Kikuu cha Iringa maeneo ya
mtaa wa Ngome mbele ya duka la Ngailo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali
hiyo ni kwamba ajali hiyo ilisababishwa na dereva wa taxi T 301 AKX aliyekuwa
akiingia barabarani kutoka pale alipokuwa ameegesha kwa nia ya kugeuza bila
kuangalia nyumba ya gari lake.
Walisema kuwa dereva huyo
aliingia barabarani kwa mbwembwe bila kuangalia pande zote kumbe nyuma yake
kulikuwa na gari lililokuwa katika mwendo kasi likielekea katika chuoni kisha kumuingia
kwa mbele.
Katika ajali hiyo hakuna
aliyekufa wala aliyeripotiwa kujeruhiwa ambapo gari lenye namba za usajili T 434 CEL lilikuwa na watu wa nne kuhu gari lingine likiwa na mtu mmoja aliyekuwa akiliendesha.
No comments:
Post a Comment