![]() |
| Rais Jakaya Kikwete |
OFISA mtendaji wa mtaa wa Ngome
Eliquis Ngakonda amewatibua wakazi wa mtaa huo kutafuna fedha za michango
waliokuwa wakichanga kwa ajili ya ulinzi wa sungusungu na ujenzi wa vyoo vya
shule ya Mshingi Tumaini na kudaiwa kuhamishwa kinyemela ili kuficha dhahama
inayomkabili.
Hayo yalibainika jana katika
mkutanop wa hadhara wa mtaa huo ul;iofanyika katika viwanja vya Soko jipya la
mtaa huo linaloendelea kujengwa huku mtuhumiwa huyo akishindwa kuhudhuria
mkutano huo.
Katika tuhuma hiyo wamo baadhi ya
mabalozi akiwemo mwanamke Prisca Mkusa ambao wanadaiwa kushirikiana na mtendaji
huyo kupita mitaani kuchangisha fedha na kuziweka mifukoni mwao huku kusudio la
michango hiyo likishindwa kutekelezeka.
Ajenda ya usafi wa mazingira
ndiyo iliyoibua hayo baada ya wananchi kutaka kujua taratibu za kuwa na sehemu
maalum za kutupa taka ili ziweze kusombwa kwa ajili ya kuyaweka mazingira safi tofauti na sasa
ambapo taka zinatupwa hovyo na kuzagaa mitaani.
Wajumbe walitaka ufanyike
utaratibu wa kujenga sehemu maalum za kutupa taka ili gari likifika ziweze
kupakiliwa ndipo ilipoibuka hoja ya kujua makusanyo ya michango ya sungusungu
ili ufanyike utaratibu wa kuona namna sehemu hizo zitakavyo jengwa.
Wajumbe walitaka mabalozi waeleze
michango yao
walikoiweka kutokana na sungusungu kutofanya kazi na kuwalazimu mabalozi
waliokuwepo kuwaeleza wananchi kuwa walimkabidhi Ngakonda na Mkusa ambao
walisema ndiyo wasimamiaji.
Hata hivyo ikagundulika baada ya
kujua walichokifanya wakaukimbia mkutano huo ikashindikana kupata majibu haraka
na wakalazimika kuwaagiza baadhi ya viongozi wa mtaa huo akiwemo mwenyekiti
kuhakikisha wanawaita watuhumiwa na kuita mkutano wa dharura mwishoni mwa mwezi
huu.
Mabalozi waliokuwepo walitaja
fedha walizomkabidhi Ngakonda na Mkusa na kufikia zaidi ya shilingi laki mbili japo kuwa huenda zikaongezeka kutokana na mabalozi wengine kutokuwepo katika mkutano huo wanaodaiwa kukusanya fedha
nyingi zaidi.
Ubadhilifu huo ulikuja baada ya
ofisa mtendaji huyo akishirikiana na viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM)
kumsimamisha uenyekiti Elizabeti Mkayula aliyeonekana kufuatilia kwa ukaribu
masuala ya kijamii ambayo yanahusu fedha za wananchi.
Hata hivyo ilielezwa kuwa
mtendaji huyo alikuwa anawatumia zaidi vinara wa kuchangisha michango hiyo
ambao ni Prisca Mkusa na Abubakari Muumba ambao baada ya kuchangisha fedha hizo
kwa kushirikiana na ofisa huyo walizitia kwenye mifukoni mwao huku wananchi
wakiambulia patupu.
Baadhi ya wajumbe waliokuwepo
kwenye mkutano huo waliongea na mtandao huu baada ya mkutano kuwa tatizo ni kwamba ofisa huyo
anafanya kazi za CCM badala ya kazi anayopaswa kufanya ndiyo maana anafanya
udanganyifu wa wazi kwa kujidai kuwa hatafanywa chochote kwa kuwa wapo wa
kumkingia kifua.
“Unajua tatizo linalokuja hapa!
Watendaji wengi wanafanya kazi za chama badala ya kazi wanazotakiwa kuzifanya.
Viongozi wa CCM walimsimamisha huyu mama uenyekiti kwa sababu alikuwa kikwazo
kwao wanapotaka kuiba maana huyu mama ni mkali na ni muwazi lakini baada ya
kufanikisha kuiba walichokusudia sasa ndiyo wanamrudisha madarakani tena. Hata
huu ujenzi wa soko haturidhiki nao kwa sababu mambo wanayoyafanya ni uchafu
mtupu. Tunaumia sana
sisi wanyonge.
“Mimi ni mwanachama wa CCM lakini
kwa hili, sipo tayari kulifumbia mamcho. Tatizo la CCM, mtu akiwa mkweli katika
chama ni adui lakini mtu mwizi na muongo katika chama ni hazina kwa sababu hiki
chama tukubali tu kuwa kimekuwa ni chama cha wezi, mafisadi na wahuni. Chaguzi
za miaka ijayo hatuponi maana tumeshaharibu kila kona” kilisema chanzo chetu
kilichoomba jina lisiandikwe.
Kuna tetesi kuwa mtendaji huyo alihamishwa na nafasi yake amebadili mtendaji mwingine Gannzan Godson jambo ambalo wqnanchi wanataka kama ni kweli wanataka makabidhiano yao yafanyike mbele yao ili tuhuma zinazomkabili azijibu.
Dodson alipoulizwa juu ya ukweli huo alikiri kuwa ni kweli na kwamba hajakabidhiwa vitendea kazi japo kuwa ameambiwa aendelee kufanya kazi katika mtaa huo.
Wakati huo huo bwana afya wa Kata
ya Kihesa Gaudence Haule ameingia katika kashfa ya kuwahadaa wakazi wa mtaa huo
huku wananchi wakiahidi kumshughulikia pale atakaposhindwa kutimiza ahadi zake
kwenye mtaa.
Katika mkutano huo ambao wananchi
walionekana kuwa na jazba juu ya viongozi waongo, bwana afya wa Kata hiyo
alikuwa na maswali ya kujibu lakini hakuwepo kwa kile kilichoelezwa na wananchi
kuwa amekimbia kujibu uongo aliowadanganya.
Mkutano huo uliazimia kuwa
mwishoni mwa mwezi Novemba aletwe ofisa huyo, ofisa mtendaji wa kata, mabalozi
ambao hawakuhudhuria mkutano wa juzi ili wawekwe kapuni, diwani wa kata hiyo,
mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Tumaini na Mwalimu Mkiuu wa shule hiyo
ili wasaidie kutoa ufafanuazi wa mambo mbalimbali.
Mkutano huo uliahilishwa hadi
Desemba Mosi mwaka huu utakapofanyika kwa ajili ya kupata majibu kwa watuhumiwa
hao.

No comments:
Post a Comment