WAKRISTO
nchini wametakiwa kutambua kuwa uongozi ni huduma ambayo ni haki ya kila mmoja
kupata bila masharti magumu na kupata mahitaji kadiri ya makubaliano ya nafasi
za huduma.
Kauli
hiyo imezungumzwa leo na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu
Tarcisius Ngalalekumtwa alipokuwa katika maadhimisho ya Misa Takarifu iliyokuwa
kwa ajili ya kufunga Mwaka wa Imani kijimbo iliyofanyika katika viwanja wa
Kichangani jimboni Iringa.
Mhashamu
askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa jimbo la Iringa na Msimamizi wa
Kitume katika Jimbo Kuu la Songea amesema baadhi ya wakuu wa mataifa huwatawala
kwa nguvu watu wao na kuwakosesha amani na haki huku wengine wakiishi kwa
wasiwasi.
“Tunapofunga
mwaka wa imani tunapata nafasi ya kutafakari dhana ya utawala na uongozi bora. Wakuu
wa mataifa huwatawala kwa nguvu. Wengi wanaotafuta uongozi, huingia katika
kinyang’anyiro cha kutafuta madaraka na wengi wao huiongia kwa kutafuta maslahi
binafsi” amesema askofu Ngalalekumtwa.
Amesema
binadamu anadaiwa kufanya marekebisho ya maisha kwa kuishi kadiri ya maagizo ya Mungu kwa kuishi kwa
amani na upendo kwa kutanguliza haki na kuwajibika ipasavyo kwa wengine.
“Uongozi
ni kuwatanguliza wengine katika mawazo na katika utendaji. Uongozi ni utii na
utumishi mwema” amesema.
Amesema
viongozi wa njanja zote wanapaswa kufanya tathmini ya utawala wao na kufanya
marekesho pale walipokosea na kuwakwaza wale waliopa dhamana hiyo.
Amesema
kila wakati kutawala kwa mabavu ni kuleta mvutano na kuwavuruga watu duniani na
kuwafanya kuishi bila amani kinyume na mpango wa Mungu anayependa watu wote
duniani waishi kwa amani, upendo na kuheshimiana.
Adhimisho
hilo
limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali na kuhusisha Parokia zote 37
za Jimbo la Iringa.
No comments:
Post a Comment