![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapt. Aseri Msangi akifungua warsha ya uhamasishaji wa uanzishwaji wa Mfuko wa afya ya Jamii Tiba kwa Kadi (TIKA) mji wa Njombe hivi leo. |
![]() |
| Wadau mbalimbali wa mji wa Njombe wakifuatilia mjadala wa uanzishwaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii Tiba kwa Kadi (TIKA). |
![]() |
| Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF) Mkoa wa Ruvuma, Ndg Silivery Mgonza akiwasilisha maada juu Usimamizi na Matumizi ya fedha za TIKA |
![]() |
| Sekretarieti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikinukuu dondoo na maoni muhimu kutoka kwa wadau, Halmashauri ya Mji wa Njombe, katika kikao cha uanzishwaji wa TIKA. |
MKUU wa Mkoa wa Njombe Kapt.
Aseri Msangi amewataka wadau mbalimbali wa Halmasahuri ya Mji wa Njombe, kuunga mkono mpango wa
Mfuko wa Afya ya Jamii Tiba kwa Kadi (TIKA) ili kutoa fursa kwa wananchi kuchangia huduma za matibabu kabla ya kuugua, kwa kuwa si wakati wote wananchi wanapougua wanakuwa na fedha kwa ajili ya kuchangia huduma hizo.
Msangi amesema hayo leo katika
ukumbi wa Kyando mjini Njombe wakati akifungua mafunzo kwa ajili ya uanzishaji
wa Mfuko wa Afya ya Jamii Tiba kwa Kadi (TIKA) yaliyoshirikisha wadau
mbalimbali wa afya Halmashauri ya Mji Njombe.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amesema mpango huu wa Tiba kwa
Kadi ni utaratibu ambao unazihusu Halmashauri za Manispaa na Miji na lengo ni kumwezesha mwananchi mmoja mmoja kuchangia
gharama za matibabu tofauti na ule wa vijijini (CHF) ambao mchango wake ni wa
kaya.
Amesema pia wadau kupitia Halmashauri
wanapaswa kushirikisha jamii katika mpango wa uanzishwaji wa mfuko huo ili
jamii iweze kupata elimu na kuwa tayari kuchangia kwa ajili ya kuboresha
huduma za afya.
Pia amesema Mfuko wa Afya ya
Jamii Tiba kwa Kadi utaiwezesha Halmashauri ya Mji Njombe pindi wananchi watakapokuwa
wamechangia mchango wa Tika, watapata jazilizo la fedha za tele kwa tele kutoka Serikalini
kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
“Fedha hizi za Tele kwa Tele
zitasaidia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika maeneo ya kutolea huduma za
afya hususani Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya” amesema.
Katika kusisitiza umuhimu wa TIKA kwa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Meneja wa CHF,
kutoka Makao Makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Ndg Constantine Makala amesema mpango huu umeanzishwa ili kuwasaidia wananchi ambao hawako katika mfumo rasmi wa ajira kwa mfano wakulima,wavuvi, wajasiriamali, wafugaji na wengineo kupata huduma za Bima ya Afya.
Ili malengo yaliyoainishwa na Serikali ya kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2015 kama yalivyoainishwa na Ofisi ya Mkoa wa Bima ya Afya, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amemalizia kwa kuhimiza Watendaji wa Mitaa na Vijiji kupewa malengo ili kufikia matokeo makubwa sasa katika sekta ya afya.
Mafunzo haya yamejumuisha wadau
mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata, Kamati ya uendeshaji wa Huduma za Afya (CHMT), wakuu wa Idara (CMT), Wajumbe wa Bodi ya Afya (CHSB), watu mashuhuri na Maofisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii.





No comments:
Post a Comment