![]() |
| Msafara wa Dkt. Slaa ukiwasili uwanjani. |
![]() |
| Uwanja ulijaa hasa. Watu zaidi ya laki moja walihudhuria. |
Ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa kiafrika kupewa mapokezi makubwa ambayo Dkt. Slaa ameyapokea katika ufunguzi wa mchezo wa mpira maarufu kama football.
Dkt. Slaa alialikwa na Chancellor pamoja na Rais wa chuo kikuu cha Alabama kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo baina ya Alabama na Georgia State.
Kiongozi huyo wa Chadema alipokewa na viongozi wa ngazi mbali mbali wa kitaifa na wa jimbo la Alabama.
Akimkaribisha Dkt. Slaa katika chakula cha asubuhi kiliyoandaliwa kwa ajili yake, Chancellor wa chuo hicho, amemfananisha Dkt. Slaa na Nelson Mandela kutokana na juhudi zake za kupambana ufisadi nchini Tanzania.
“Tunajua jinsi polisi wanavyowaua raia na kuwakamata wapinzani” alisema kiongozi huyo" alisema kiongozi wa Alabama.
Kadhalika kiongozi huyo amemsifu Dkt. Slaa kutokana na msimamo wake, sera zake za kulikomboa Tanzania kutoka katika umasikini licha ya chama chake kutungiwa kesi za ughaidi.
Kwa upande wake, wakiwa kama moja ya vyuo vikuu nchini marekani, wako tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Dkt. Slaa hasa katika sekta ya elimu.
Wamemuomba ajisikie nyumbani na kufurahia mchezo wa American football. Kwa unyenyekevu Dkt. Slaa aliwashukuru governor, na viongozi wengine kwa kuwa wakarimu sana kwake na mkewe na watu wa Tanzania.
Dkt Slaa amefurahishwa jinsi wamarekani wanavyokuwa na hamasa na kuipa kipaumbele michezo. Nimejifunza kwamba michezo ni moja ya mbinu ya kuiunganisha taifa hasa wakati wa changamoto.
Kadhalika amesema kwamba, chama chake cha Chadema kina sera ya kukuza vipaji kupitia taasisi za michezo nchini Tanzania na siyo kuwaleta Makocha wa kigeni, mmoja baada ya mwingine na kuwapeleka Ikulu kula pilau na kupiga picha.
"Nilichojifunza ni kwamba, lazima nirudi na ujumbe kwa watanzania kuweka mifumo endelevu ya michezo kuanzia shule za misingi hadi vyuoni. Nilichoona hapa ni mfano wa kuigwa" aliksema Dkt. Slaa.


No comments:
Post a Comment