masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, September 17, 2013

BREAKING NEWS: BALOZI WA CHINA ASHTAKIWA UMOJA WA MATAIFA

Balozi wa China nchini, Dk. Youging (kulia) akiwa kwenye mkutano wa CCM. Kulia ni Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana. (katikati)


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wapeleka mashtaka rasmi kumshtaki Balozi wa China kwa umoja wa mataifa (UN).

Balozi wa china hapa nchini Dkt. Lu Youging ameshtakiwa rasmi hii leo na Chadema kwa umoja wa matifa kwa kile kilichoelezwa kuwa anafanya uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinyume cha makubaliano ya sheria za umoja wa mataifa ya mwaka 1961 kuwa ni kosa kwa Balosi yeyote kufanya siasa katika nchi isiyo ya kwake.

Mashtaka hayo yamekuja siku moja baada ya Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chadema, Ezekia Wenje, alipozungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa Balozi huyo amevunja mkataba unaowaongoza mabalozi ujulikanao kama ‘Vienna Conversion on Diplomatic Relations’.

Wenje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana, mkoani Mwanza, alisema mkataba huo unazungumzia mahusiano ya kibalozi baina ya nchi na nchi na kazi za balozi awapo kwenye nchi fulani kwamba siyo kujihusisha na mambo ya ndani ya nchi husika zaidi ya kujenga mahusiano baina ya nchi hizo na kusaidia wananchi wa nchi yake na wananchi husika wanaotaka kwenda kwenye nchi yake.

“Ibara ya 41 (1) inakataza mabalozi kujiingiza katika masuala ya ndani ya nchi ikiwamo siasa, ibara ya tatu ikionyesha kazi za balozi na ibara ya 31 (1) inazungumzia kinga ya balozi, kama atajiingiza kwenye kazi ambazo hazimuhusu kinga itaondolewa,” alifafanua Wenje.

Alisema kazi ya balozi ni kutengeneza  uhusiano baina ya nchi yake na Tanzania na siyo kuwa mwenezi wa chama chochote cha siasa na kwamba alichofanya balozi huyo ni kugeuka kuwa Katibu Mwenezi wa CCM huku akisakata muziki wa chama hicho hadharani.

Alisema kimsingi, balozi huyo hakutakiwa kushiriki kwenye mkutano huo na mikutano anayopaswa kushiriki ni ya kiserikali, lakini alisimama kuhutubia wananchi akiwa amevaa sare ya CCM.


“Tusingependa uhusiano wa kihistoria kati ya China na Tanzania ambao umedumu kwa muda mrefu tangu uhuru uingizwe matatani au shakani kwa sababu ya mapenzi binafsi ya balozi kwa CCM,” alisisitiza Wenje.

Balozi huyo alikaririwa na vyambo vya habari wakati akihutubia mkutano wa hadhara akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na kujitahidi kuwasalimia wananchi hao kwa lugha ya kabila la Wasukuma kwa kusema mwadila.
Alisema pamoja na Tanzania kuwa na mfumo wa vyama vingi, anaamini kuwa CCM bado iko imara na inaweza kuendelea kuongoza kwa muda mrefu.
“Kwa hili inadhihirisha kuwa hakuna chama kama CCM kutokana na uimara wake na hili wanalofanya sasa la kuja kuimarisha chama nasi kule China kupitia chama chetu tawala cha CPC (Chama Cha Kikomunisti cha China), tunafanya kama hivi pia. Mwadila, Shinyanga, CCM Oyeeeeee asanteni sana,” alikaririwa akisema.

Wakati huo serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, imesema kuwa kitendo kilichofanywa na Balozi huyo siyo sahihi na kinakiuka mkataba wa Vienna.

“Wizara inapenda kutamka kwamba kitendo cha Balozi yoyote kuhudhuria mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kuvaa sare zenye nembo ya vyama vya siasa siyo sahihi na kinakiuka Kifungu cha 41(1) cha Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961, unaoongoza uhusiano wa kidiplomasia,” alisema Membe katika taarifa yake jana jioni.

Taarifa hiyo ilisema kuwa mkataba huo unazuia wawakilishi wa nchi za nje kujihusisha na ushabiki wa kisiasa wanapofanya kazi zao kwenye nchi za uwakilishi.

“Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012, Wizara ilikumbana na vitendo vinavyofanana na kitendo hiki na ikachukua hatua stahiki, kadhalika kwa tukio hili Wizara itachukua hatua za kidiplomasia zinazostahili ili kuzuia jambo hili lisitokee tena,” alisisitiza.

Alisema Wizara imeona picha na habari kwenye vyombo vya habari zikieleza na kumuonyesha Balozi huyo akiwa kwenye mkutano wa CCM

Balozi huyo alikwenda wilayani humo kuhudhuria uzinduzi wa mradi wa viwanda vya kuchambua pamba vinavyojengwa na mwekezaji wa Kichina anayeitwa Tahong ambapo viwanda hivyo vinatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchambua tani 120,000 za pamba kwa mwaka vitakapokamilika mwakani.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipotafutwa kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo, hakupatikana kutokana na simu zake za kiganjani kufungwa.
Hata hivyo, Nape juzi alisema atatoa ufafanuzi wa masuala yote kuhusu chama chake atakaporejea kutoka katika ziara hiyo anayofuatana na Kinana.

No comments:

Post a Comment