masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Friday, August 9, 2013

MILIONI 10 KWA TAARIFA WASHUKIWA WA ZANZIBAR

Kristie Trup na Katie Gee


Polisi nchini Zanzibar wameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni 10 za Tanzania kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa watu waliowashambulia wasichana wawili waingereza kwa Tindikali.

Wasichana hao kutoka London, Kirstie Trup na Katie Gee, walirushiwa Tindikali kwenye nyuso zao walipokuwa wanatembea mjini Jumatano Jioni.

Serikali ya Zianzibar ndio itakayotoa zawadi hiyo.

Polisi wanasema kuwa hizo ni pesa nyingi sana kisiwani Zanzibar.

Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa miaka 18 kutoka London, walipelekwa hospitalini nchini Tanzania baada ya kushambuliwa Mashariki mwa kisiwa hicho.

Inaaminika kuwa walitoka Tanzania kuelekea Uingereza Alhamisi usiku.

Mama za wasichana hao, Rochelle Trup na Nicky Gee, walielezea kughadhabishwa mno na shambulizi hilo ambalo sababu yake haiwezi kujulikana na ambalo halikuchochewa kivyovyote.

Walishambuliwa na wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki.

Polisi walisema kuwa walirushiwa Acid kwenye nyuso zao, kifuani na kwenye mikono yao walipokuwa wanatembea mjini .

Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliowashambulia walitoroka na polisi hawajui kwa nini wanawake hao walilengwa.

Mama za wasichana hao walisema kwenye taarifa yao kuwa walighadhabishwa mno na shambulizi hilo na hawaelewi kwa nini wasichana hao walishambuliwa ili hali walikwenda Zanzibar kwa nia njema.

''Tunashukuru kwa wale wanaotaka kujua kinachoendelea lakini tungeomba vyombo vya habari vituwache kwa sasa hadi tutakapokutana na watoto wetu,'' alisema msemaji wa familia za wasichana hao.


Wasichana hao walikuwa wamekaa Zanzibar kwa muda wa wiki mbili ingawa walitarajiwa kuwa huko kwa wiki tatu, kupitia kwa kampuni ya usafiri ya i-to-i Travel, ambayo ilisema inafanya kila iwezalo kuwarejesha nyumbani Uingereza.


Chanzo: bbc swahili

No comments:

Post a Comment