masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, July 24, 2013

WANAKIJIJI CHA IHEMI WAMTIMUA MWENYEKITI WAO


Maelezo ya benki juu ya fedha za kijiji cha Ihemi zinazodaiwa kukwapuliwa na mwenyekiti wa kijiji hicho.

MWENYEKITI wa kijiji cha Ihemi Kata ya Mgama Wilaya ya Iringa vijijini Castory Likwiluka amevuliwa madaraka kutokana na matumizi yake mabaya ya madaraka kutumia mali za kijiji bila idhini ya wanakijiji.

Katika mkutano uliofanyika kijijini hapo leo wanainchi walilazimika kumpumzisha mwenyekiti huyo ili kulinda mali za kijiji zisitumike vibaya kwa maslahi binafsi.

Miongoni mwa tuhuma zilizomuondoa madarakani ni kutumia muhtasari bandia na kuchukua pesa benki kiasi cha shililingi 840,000/= pamoja na shilingi 450,000/= za ulinzi wa nguzo za umeme gredi ya taifa ambazo kampuni ya umeme (TANESCO) hulipa kijiji kwa ulinzi na kufikisha jumla ya shilingi 1,290,000/= ambazo mwenyekiti huyo ametumia bila ridhaa ya wananchi.

Akisoma tuhuma za mwenyekiti huyo kwenye mkutano, Euzebio Nyalusi amesema mwenyekiti huyo amekuwa na kawaida ya kuamua mambo bila kuwashirikisha wananchi na kufanya kijiji kama mali yake binafsi.

“Mwenyekiti ameuza mashamba ya kijiji bila kuwashirikisha wanakijiji. Licha ya kuwa mashamba yalishatolewa hukumu na kuamriwa yarudishwe katika kijiji, mwenyekiti huyu ameyauza tena” amesema.

Pamoja na hayo wananchi walihoji mchango wa wawekezaji katika kijiji licha ya kuwa na wawekezaji sita ambao bila mikataba yao kujulikana kwa wananchi.

“Hapa kijijini kuna wawekezaji wapatao sita lakini hatujui mchango wao. Ina maana kijiji hakina mkataba nao? Hatuoni faida ya kuwa na wawekezaji ambao hawana msaada wowote” amehoji.

Wananchi wamemlalamikia mwenyekiti huyo anasadikiwa kuuza tofari walizofyatua kwa ajili ya kujengea shule ya sekondari ya kata ya Mgama ambapo haijulikani idadi kamili ya tofari zilizopelekwa shuleni hapo.

“Tunataka kujua tofari tulizofyatua kwa ajili ya ujenzi wa shule zimekwenda wapi? Haya ni matumizi mabaya ya nguvu za wananchi. Tunatumiwa kwa ajili ya watu binafsi na si maendeleo ya kijiji kama inavyokusudiwa. Kwa mtindo huu hatuwezi kufika popote” amesema na kuhoji.

Alipopewa nafasi ya kujibu tuhuma hizo, Likwiluka alikiri kuwa na mapungufu hayo na kusema ni ubinadamu tu huku akiomba wananchi wamsamehe.

“Ni kweli kwamba hizo tuhuma zinanihusu lakini ni ubinadamu tu. Pesa zimeshatumika na hayo mengine kwa 
 kweli naomba mnisamehe” amesema.

Licha ya tuhuma hizo kuelekezwa kwa mwenyekiti, wananchi wamedai kuwa hata ofisa mtendaji wa kijiji Aloyce Mduda anahusika kwa kuwa naye ni miongoni kwa waliotengeneza muhtasari bandia na kuhidhinisha fedha kuchukulia benki.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa Mduda aliwahi kutuhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha za kijiji cha Kiwele na kuhamishiwa katika kijiji cha Ihemi ambako nako ameingia katika kashfa hiyo.

Wananchi wamelazimika kumteua mwenyekiti wa muda Ezekiel Mlyuka hadi uchaguzi utakapofanyika ili kuwezesha shughulizi zingine kufanyika.


Hata hivyo mtandao huu umefanikiwa kupata maelezo ya benki (bank statement) inayoonesha kijiji hicho kuchukua fedha Mei 14, 2013 kwa Cheki (CHQ) No 218610 kiasi cha shilingi 840,000/= wanazozilalamikia wananchi.

No comments:

Post a Comment