masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, July 24, 2013

UTAPIAMLO, LISHE DUNI SUMU KWA WATOTO


WATOTO 43,000 wenye umri chini ya miaka mitano nchini hufa kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya ukosefu wa lishe pamoja na kukosa vitamini A.

Upungufu mkubwa wa vitamini A unaweza kusababisha kuharibika macho na ni sababu inayoongoza ya kupofuka macho utotoni.

Kuanzia mwaka 2000, kampeni ya mara mbili kwa mwaka ya kutoa vitamini A ya ziada na dawa za kuua minyoo inafanyika japo kuwa vifo bado vinaendelea kutokea.

Kuendelea kwa vifo hivyo kunasababishwa aidha na uwajibikaji wa wazazi au walezi kuwapeleka watoto wao katika chanjo au elimu ya chanjo hiyo kutowafikia wananchi.

Manispaa ya Iringa nayo hupoteza watoto wengi, jambo linaloendelea kubaki kama changamoto kwa wazazi, walezi na wadau mbalimbali wa afya katika kupambana na vifo hivyo japo kuwa takwimu zinaonesha kupungua.

Mwaka 2009 Manispaa ya Iringa ilipoteza watoto 227 chini ya umri wa miaka mitano, mwaka 2010 jumla ya watoto 164 wakati mwaka 2011 jumla ya watoto 126 walikufa.

Katika kuendelea na mapambano haya manispaa imejipanga kutoa elimu kwa wazazi na walezi ili kuweza kuwafikisha watoto wao katika vituo vya afya kwa ajili ya kupatiwa matone ya vitamini A.

Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo May Alexander katika mazungumzo na gazeti hili ofisini kwake anasema vifo vya watoto chini ya umri huo vimeendelea kuwa tatizo.

Anasema kutokana na hilo ndiyo maana tarehe 27 na 28 Desemba huwa ni siku ya utoaji wa matone kwa watoto na vidonge vya minyoo huku akiwataka wazazi na walezi kutowaacha watoto wao majumbani.

“Ni watoto wachache ambao wanapata maziwa ya mama wengine wanakosa vyakula vyenye vitamini A. Wazazi na walezi tuna jukumu kubwa la kushirikiana katika suala hili kutokomeza vifo hivi kwa kuwapeleka watoto katika vituo vya afya kwa ajili ya chanjo na matone,” anasema.

Anasema miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili nchi kutokana na vifo hivyo ni utapiamlo ambapo changamoto hii ni kubwa si kwa Tanzania pekee bali kwa nchi mbalimbali duniani.

Watoto 43,000 wanaofariki nchini kila mwaka ni sawa na wastani wa mtoto mmoja kufa katika kila dakika 12.

Pindi mtoto mwenye utapiamlo anapougua kuharisha, malaria au homa ya mapafu anakuwa na uwezekano mkubwa wa kufariki dunia.

Vifo vyao vingeweza kuepukika iwapo watoto hawa wangelishwa vyakula vyenye ubora wa kutosha.

Ingawa utapiamlo husababisha vifo, ni kwa nadra sana vifo hivyo kusababishwa na kushinda njaa.

Kwa mujibu wa Alexander, watoto wanakufa kwa sababu milo yao haina virutubisho vya msingi vinavyohitajika kujenga mfumo imara wa kinga za mwili na kuwaweka wenye afya.

Katika muongo (miaka 10) uliopita, zaidi ya watoto 600,000 wenye umri chini ya miaka mitano wanakisiwa kufa kwa kukosa lishe ya kutosha.

Anasema idadi ya vifo vilivyotokana na utapiamlo tangu mwaka 2000 vinaweza kulinganishwa na vifo vilivyotokea kwenye mauaji ya kimbari huko Rwanda na vifo vilivyotokana na tsunami na tetemeko la ardhi Hai kwa pamoja, matukio ambayo yaliishitua sana dunia.

Ingawa watu walihamasishwa kukabiliana kuyapa umuhimu mkubwa mauaji ya kimbari na yale ya tsunami, utapiamlo umebaki ukipuuzwa huku ukiendelea kuongeza kasi ya kuteketeza watu. Utapiamlo unadhoo?sha uchumi.
Wakulima na wafanyakazi wengine, hasa wanawake, wanadhoo?ka na kudumaa, kutokana na kukosa vyakula viletavyo nguvu mwilini pamoja na maradhi ya upungufu wa damu.

Kutokana na utapiamlo, wakulima hushindwa kutumia nguvu nyingi hivyo kusababisha mavuno kupungua.
Utapiamlo pia unachangia upotevu wa fursa za kiuchumi, kwani watu wazima wenye ukuaji uliodumaa wa ubongo kutokana na kukosa virutubisho kipindi cha utoto wana uwezo mdogo wa kubuni na kuchangamkia fursa mpya za soko.
Upungufu wa virutubisho pekee hugharimu Tanzania sh bilioni 700 kila mwaka.

Alexander anasema katika kila watoto 1,000 wanaozaliwa, watoto 3.1 wanazaliwa wakiwa na tatizo la mishipa ya fahamu kwa sababu ya kukosa Foliki Asidi (NFFA 2009). Na watoto milioni 4.2 na wanawake 4.3 wana upungufu wa madini ya chuma (IHI 2009).

Vitamini A ni vitamini ambazo zinahitajika machoni ili kuongeza mwanga.

Ili vifo vya watoto viweze kupungua na kwisha, anasema inabidi mamlaka husika zitekeleze na kuwajibika kwa nafasi yake kwa ushirikiano wa wazazi na walezi.

Isitoshe bila taarifa sahihi kuhusu faida za kuwanyonyesha watoto kikamilifu na kukosekana kwa vyakula vilivyorutubishwa madukani, watu hawawezi kutarajiwa kuchukua hatua hizo zenye manufaa.

Katika hali hii ambayo maisha ya watu 43,000 yapo hatarini kupotea, elimu ya afya ni muhimu katika kuepuka uchumi kuathirika, taifa halistahili kuendelea kupuuza lishe.

No comments:

Post a Comment