![]() |
| Onesmo Olengurumwa |
WANDISHI wa habari, Wanaharakati na Viongozi wa mashirika
yasiyo kuwa
ya Kiserikali wameombwa kuunganisha nguvu zao na
kuendelea kuyatetea kwa uhakika makundi yanayohitaji huduma yao .
Wito huo umetokewa na afisa Habari wa Mtandao wa
Kutetea haki za Bianadamu Tanzania
(Tanzania Human Rights Defenders Coalition-THRDs Coalition) Bw. Elias Mhegera wakati akiongea na
waandishi wa habari na viongozi wa mashirika yasiyo kuwa ya Kiserikali
Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma .
Mhegera ambaye amefuatana na Mratibu Taifa wa
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (Tanzania Human Rights
Defenders Coalition-THRDs Coalition) katika ziara ya
utafiti wa kuangalia vikwazo na changamoto ambazo zimekuwa zikiwakwaza
watetezi wa haki za Binadamu nakuona njisi gani watawasaidia na
kufanya shughuli zao zinakwenda vizuri.
Alisema lengo la ziara yetu katika Mikoa ya
Tanzania Bara na Visiwani zikiwa ni juhudi za Mtandao huo kufanya utafiti na
kuyatambua matatizo, vikwazo na changamoto mbali mbali za
ukandamizaji wanavyofanyiwa watetezi hao wa haki za binadamu
ambavyo makundi hayo yamekuwa kifanyiwa huku vyombo vilivyo pewa
mamlaka na serikali kuwalinda vikiwa havitoi majibu wala kutafuta
mwarubaini wa kuvikomesha.
Bw.Mhegera ambaye katika maelezo yake alitolea
mfano wamatukio ya kinyama waliyofanyiwa Mwenyekiti wa jukwa la
wahariri Tanzania Absalom Kibanda na Dkt. Steven Ulimboka aliendelea
kufafanua kuwa hivi sasa Mtandao huo umejipanga kuanza kutoa mafunzo na
mbinu za kujikinga kwa wahanga wa vitendo hivyo pamoja na kuandaa
mikakati mbalimbali ya kuwatete kwa kuwawekea wanasheri na kuhakikisha
kuwa mkono wa Sheria unawanasa maharamia hao.
Akichangia kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa
Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilayani Tunduru (MATU) ambaye pia
Focal Person wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Kanda ya Kusini Pwani
Bw. John Nginga alisema kwamba changamoto zinazo wakabili kama
watetezi wa haki za binadamu ni pamoja na vitisho kutoka kwa viongozi
wa serikali,kutopata ushirikiano katika kutekeleza majukumu na kupata
taarifa sahihi kama
upatikanaji wa takwimu ikiwemo masuala ya sharia
mbali mbali za nchi hususan zinazolengwa haki za binadamu.
Aliendelea kueleza kwamba pamoja na changamoto
zinazowakabili kama Mtandao bado hawajakata taa katika kupigania haki
za Binadamu hasa katika masuala ya utetezi kwani wananchi
waliowengi hususan waishio vijijini wamekuwa wakikwama sana katika upataji wa
huduma na haki za msingi za kihuduma kama Wanawake, Wajane, Watoto,Walemavu
na WAVIU
Kwa mujibu wa Bw. Mhegera ziara yao ilianzia
Unguja, Pemba Tanzania Visiwani na baadae katika Mikoa ya Arusha, Ngorongoro, Serengeti, Musoma, Bunda,
Mwanza, Tabora, Kigoma na Katavi,Rukwa,Mbeya,Iringa na sasa Ruvuma ambako
alisema katika msafara huo wamebaini kuwepo kwa Vikwazo na changamoto
mbali mbali zinazo hitaji kutolewa kwa elimu ya uhakikwa kwa jamii
hapa nchini.
Akitoa neon la shukrani baada ya kufungwa kwa
kikao hicho mwakirihi wa asasi ya Kiraia yakitengo cha Kiislam kinacho
shughuliki amasuala ya Ukimwi Wilayani Tunduru (BAPRO) Issa Mdaraka
alisema kuwa endapo jamii na viongozi wa Mashirika ya kijamii yatapatiwa
elimu hiyo upo uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa mabadiliko ya
kuachana na mila na destuli za aina hiyo.

No comments:
Post a Comment