masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, June 30, 2013

VIKUNDI VYAONYWA KUJIPENDEKEZA KWA WANASIASA




WANACHAMA wa vikundi vya akiba na mikopo wameonywa kuacha utegemezi na kuwa ombaomba kwa wanasiasa kwa madai kuwa tabia hiyo inachangia vikundi vyao kushindwa kujiendesha na hivyo kufa mapema baada ya misaada kusitishwa.

Mratibu wa benki za wananchi waishio vijijini (VICOBA) Tisiana Kikoti ametoa ushauri huo ja wakati wa uzinduzi wa kikundi cha Lugodalutali katika  Kata ya Igombavanu Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Kikoti alisema vikundi vingi vimekuwa vikiwategemea wanasiasa jambo ambalo linaweza kuleta athari kubwa ambapo baadhi ya vikundi vingine vimekufa kutokana na uongozi wa wanasiasa hao kukoma na kuwataka wana-vicoba kujitegemea.

“Vicoba ni vyama visivyo na mlengo wowote wa kisiasa, sasa ninawasihi msiwategemee wanasiasa au misaada kuendesha vikundi vyenu, tunataka hivi vicoba view endelevu ili baadaye tuje tufungue benki za Kata, lakini kama mkiegemea kwa wanasiasa mjue wanapoondoka madarakani na vikundi vyenu vinakufa” alisema Kikoti.

Amewataka wanavikundi kuwa wabunifu katika miradi mbalimbali ya ufugaji wa kuku, na hata kilimo cha Uyoga, kwa kuwashirikisha wataalamu ili kupata mafunzo ya shughuli hizo zitakazoendesha vikundi vyao.

Hata hivyo aliwatahadharisha kuwa makini na matapeli katika kuwapokea wageni katika vyama vyao kutokana na vikundi vingi kutapeliwa na watu waoingia kama wageni.

Baadhi vya vicoba wilayani Kilolo vimetaperiwa kwa zaidi ya shilingi Milioni 30.

“Kuweni makini sana na mambo ya fedha, hasa matumizi yasiyofaa muyaepuke, lakini jambo lingine ni kuhusu wageni wanaofika hapa ninawaombeni mjihadhari sana nao kwani kuna wenzenu wa Kilolo walipokea wageni waliojitambulisha kama ni waratibu wa vicoba, wakachangishwa fedha shilingi Miliuoni 31 zilikwenda na maji, kwa hiyo muwaepuke sana watu wanaifika hapa kijijini na kujiita waratibu au wanataka muchange hela” alisema.

Mkoa wa Iringa una zaidi ya shilingi Milioni 500 zinazotokana na vicoba na vikundi 486 na wanampango wa kufungua benki ya mkoa ya Vicona huku bodi ya ufuatiliaji wa mitaji ikiendelea na mikakati hiyo ili kufanikisha shughuli za ufunguzi.

Naye ofisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Mufindi  Hatibu Bwashehe alisema vikundi vingi vinashindwa kuendelea kutokana na hali ya utegemezi, huku akiwataka wanavikundi wa VICOBA kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ili kuwa na maisha bora.

Bwashehe alisema ili kuwavutia watu wengine waingie katika vikundi vya akiba na mikopo wanachama wake wanatakiwa kuwa tofauti kimaendeleo na siyo kuwa na maisha yanayofanana na wale wasio katika vikundi.

“Ndugu zanguni, mkitaka kufanikiwa kuwavuteni hawa wasiotaka kujiunga, kwanza kuweni na nidhamu ya matumizi ya fedha ili hela mnayokopeshana iweze kufanya mambo ya maendeleo, itakuwa ni aibu kwenu kama hamtakuwa na maisha ya mfano na wengine watoto wenu wakifukuzwa shule kwa kukosa ada, hawa hawataona umuhimu wa kujiunga katika vicoba yenu” alisema Bwashehe.

Aliwataka wananchi wote kujiunga katika vikundi hivyo ili kujiondoa katika maisha duni ya umasikini na kuwa wanachama wanatakiwa kuwa makini katika kutafuta wafadhili makini ambao hawatawageuza kuwa watumwa.

Kwa upande wake mratibu wa Vicoba Wilaya ya Mufindi Scola Mitimingi alisema Wilaya ina vikundi 26 na tayari wana jumla ya akiba ya shilingi Milioni 5.4 na kuwa lengo kuu la kuhamasisha wananchi hao kujiunga katika vikundi ni kuondokana na maisha duni yanayotokana na kilimo cha jembe la mkono, kwani baada ya kupata mtaji mkubwa kila mwanachama atakopeshwa zana bora za kilimo.

No comments:

Post a Comment