masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, May 28, 2013

WAZEE WALAANI CCM NG'ANG'ANGE

Brian Kikoti akiwahutubia wananchi wa Ng'ang'ange.



Mratibu wa Chadema nyanda za juu kusini Frank Mwaisumbe akiwahutubia wananchi wa Ng'ang'ange.


Baadhi ya wananchi wa Ng'ang'ange waliofika kwenye mkutano wakisikiliza wahutubiaji.

Mratibu wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini Frank Mwaisumbe akifungua ofisi ya Kata ya Ng'ang'ange.



WAZEE wa kata ya Ng’ang’ange wamelaani vikali mfumo wa uongozi walio nao na kuwaongoza wananchi kurudisha kadi za CHAMA cha Mapinduzi (CCM) huku wakitoa shutuma nyingi kwa chama hicho.

Hayo yamefanyika juzi katika Kata hiyo wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambapo zaidi ya watu 250 walirudisha kadi za CCM na kujiunga na Chadema.

Wakiongozwa na mzee Lucian Mahenge mwenye umri wa miaka 74 waka ti wa kurudisha kadi alisema hakuna sababu ya kuendelea kuking’ang’ania chama kisicho na msaada na kwamba hakina jipya.

“Baada ya miaka 50 ndani ya CCM nimeona kuna mateso na siyo uhuru tena tulioahidiwa. Uhuru alioutafuta Baba wa Taifa umegeuka kuwa mateso kwetu sasa najiuliza imekuwa hivi kwa sababu Baba wa Taifa hayupo tena duniani? Sasa nawaomba wazee wengu, wanaume na wanawake tuungane na vijana wetu kuhakikisha mateso haya tunayakimbia ndani ya CCM” alisema Mahenge.

Alisema kumekuwa na ubaguzi uliopindukia katika utoaji huduma hali inayosababisha watu kupata tabu na kutokujua hatima ya maisha yao.

“Ndugu zangu, mimi mzee wenu ambaye tangu uhuru nipo ndani ya CCM nawaambia ukweli kuwa CCM ya Baba wa Taifa siyo hii mnayoiona leo. Huu ni mzoga. CCM ya wakati huo ilikuwa ni nzuri sana lakitu kwa sasa nimefikiri sana nikaona chama kinachoweza kutusaidia ni hiki Chadema. Tuungane kwa pamoja tuiage CCM iliyooza” alisema.

Naye mratibu wa Chadema kanda ya nyanda za juu Kusini Frank Mwaisume akimnadi mgombea wa udiwani kupitia Chadema alisema miaka 50 imekwisha watu watanzania wakiwa na uchovu kupindukia ambao sasa hakuna matumaini ya kupata ahueni kupitia serikali yao kwa kuwa nayo ina hali mbaya.

“Baba wa Taifa alilenga kulipeleka Taifa katika maendeleo na kuyafikia maziwa na asali lakini watu waliopewa dhamana hiyo wamekuwa hawana weledi ya kusimamia mlengo huo. Sasa ni wakati wa kufanya maamuzi ya kuwakataa watu wasio na sifa” alisema Mwaisumbe.

Amewataka wananchi kutokufurahia kupewa shilingi 2,000/= kwa ajili ya kumchagua kiongozi kwa sababu pesa hizo zitageuka kuwa maombolezo kwao.

“Tunamtaka diwani kwa ajili ya maendeleo haila hatumchagui diwani kwa sababu ya fedha. Ukimchagua mtu kwa sababu ya fedha unaangamiza familai yako. Usifurahi kwa kuwa unapewa shilingi 2,000/= ili umchague mtu” alisema.

Alisema mzalendo wa nchi hufanya maamuzi bila kushawishiwa kwa rushwa na kwamba mwananhi anayesaliti kata, husaliti kijiji, mtaa au kitongoji hadi familia yake na hivyo kuwataka wananchi wasimsaliti mgombea wa Chadema kwa ajili ya maendeleo kata hiyo.

Naye mgombea udiwani kwa tiketi ya Chadema Nafred Lucas Chahe amewataka wananchi wa kata hiyo kumfanya kuwa daraja ili awatumikie kwa dhati na mwisho maendeleo yaweze kupatikana.

“Tuna mambo mengi sana hapa kwetu hayajawah kutatuliwa miaka 50 iliyopita hadi leo. Mnifanye kuwa msemaji wa mambo haya ili yaweze kutatuliwa. Malengo yetu tunayopanga yatatimia tukishirikiana kwa pamoja ila tu cha msingi kunipa kura yenu ili niweze kuwa msemaji ili tufanikishe malengo yetu.

Mkutano huo ulikwenda sambamba na ufunguzi wa ofisi ya Kata ambapo imejengwa kwa jitihada za mgombea udiwani huyo.

Uchaguzi mdogo katika kata hiyo unatarajiwa kufanyika Juni 16 Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment