masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, May 30, 2013

AHADI ZA MGOMBEA WAKO ZIMETEKELEZWA?

Mbunge wa Njombe Kaskazini Deo Sanga (Japeople) akijibu maswali aliyoulizwa na mtandao huu.

VUGUVUGU la wananchi kutaka mabadiliko ili kuleta maendeleo linazidi kuchukua sura mpya katika maeneo mbalimbali mijini na vijijini baada ya wananchi kuwataka viongozi wao watimize ahadi walizowaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi.

Wananchi wa kata ya Lupembe iliyopo Mkoa wa  Njombe wamewajia  juu baadhi ya viongozi wa serikari kwa kuwataka kuwa wakweli kwa kile walichokiita kuwa ni kushindwa kutimiza ahadi zao walizoziahidi katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mwaka 2010.

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti wakazi wa kata za Mfiliga na Lupembe wamemkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza ahadi yake aliyoiahidi wakati wa uchaguzi kwamba  atakapo chaguliwa kuwa rais atakuwa na uwezo wa kuishawishi mahakama kumaliza mgogoro uliopo katika kiwanda cha chai Lupembe.

Wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Rais Kikwete aliwaahidi wananchi wa Lupembe kuwa akiwa rais atamaliza mgogoro huo wakati akiwahutubia wananchi hao kwenye mkutano uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Wanyingi.

Rais Kikwete aliahidi kuihimiza mahakama kuharakisha kutoa majibu ya kesi ya kiwanda hicho jambo ambalo halijafanyika hadi sasa huku chaguzi zingine zikikaribia kuanza.

Walisema kumekuwapo na sitofahamu juu ya utekelezaji wa ahadi hiyo na nyingine nyingi zilizotumika kuwanadi wagombea katika kipindi cha kampeni mwaka 2010 jambo ambalo linazua hofu ya kuendelea na maisha magumu kwa wananchi hao.

“Ni kweli kwamba tunatambua kiwanda cha chai Lupembe kesi yake ipo mahakamani na hatutaki rais aingilie uhuru wa mahakama bali bali tunachotka atimize ahadi yake ya kuihimiza mahakama katika kutoa haki ya kesi hiyo kama alivyoahidi” walisema.

Pamoja na kumlalamikia rais juu ya ahadi hiyo, wamemtuhumu  Mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazini Deo Sanga alimaarufu kama “Ja People” kuwa aliahidi kulishughulikia jambo hilo pindi atakapochaguliwa kuwa mbunge.

Inaelezwa kwamba Mbunge huyo alitoa ahadi hiyo mara kadhaa katika mikutano mbalimbali ya kampeni za kujinadi kwake na kwamba hadi sasa hakuna maendeleo yoyote kuhusu ahadi zake huo.

Akijibu hoja hiyo Deo Sanga  alikiri kuwa ni kweli kwamba ahadi hiyo ilizungumza katika kampeni zake na zile za Rais na juhudi za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo zinaendelea japo kuwa hakuziainisha.

“Zipo ahadi nyingi ambazo ziliahidiwa kipindi cha kampeni yangu na rais kwa wananchi wa jimbo la Njombe Kaskazini kama walivyo kueleza wananchi, lakini pia zipo ambazo tayari zimekwisha tekelezwa kwa kiwango kikubwa na nyingine bado zingali zinaendelea kufanyiwa kazi’ alisema Sanga.”

Kuhusu mgogoro uliopo kati ya mwekezaji na wakulima wa kiwanda cha chai Lupembe, alisema uamuzi wa mahakama kuhusu kesi hiyo kwa sasa ipo ukingoni.

Kiwanda cha chai Lupembe kilifungwa miaka kadhaa iliyopita kufuatia mgongaro wa kimasilahi  uliojitokeza kati ya mwekezaji Nawab Mullar dhidi ya wananchi ambao awali ndiyo waliokuwa wamiliki wa kinda hicho.

No comments:

Post a Comment