masuguru
Tangazo la cheti
tangazo
KLERUU
KLERUU
CAPRICORN
Ibada
Friday, May 24, 2013
MBIO ZA MARATHON KUTIMUA VUMBI IRINGA KESHO
MBIO za Ruaha Marathon zinatarajiwa kufanyika leo katika Mkoa wa Iringa zikishirikisha watu mbalimbali kutoka mbalimbli duniani.
Muwezeshaji wa mbio hizo Frank Mwaisumbe ameuamb kuwa tayari watuia mtandao huu kuwa zaidi ya washiriki mia moja wamekwisha kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki mchezo huo.
Pamoja na maandalizi hayo Mwaisumbe amesema wamekumbwa na changamoto mbalimbali kutoka kwa washiriki ikiwemo changamoto ya mawasiliano ambapo hawakujua ni wapi wananatakiwa kufika kujiandikisha.
Akifafanua zaidi juu ya malalamiko ya watu yaliokuwa yakizagaa mjini hapa kuwa maandalizi ya mchezo huo haeleweki, Mwaisumbe amesema malalamiko hayo yanatokana na watu wenyewe kukurupuka kufunga safari bila kuchukua mawasiliano ya kutosha kule waendako.
“Tunaweza tukawa na mapungufu sisi waandaji kweli lakini tumepata changamoto kwa washiriki wetu kwa sababu matangazo yetu yapo katika tovuti, redio mbalimbali pamoja na kwenye mitandao. Lakini mtu anapoliona tangazo hilo na kuamua kushiriki anasahau kuchukua mawasiliano yetu na pindi anapofika anapata shida kwa sababu tayari hana hata mawasiliano nasi na sisi siyo manabii kujua kama kuna washiriki kutoka sehemu fulani” amesema.
Changamoto nyingine amesema kuwa washiriki wa mchezo huo wengi ni wageni kuliko wenyeji hali inayoonesha kuwa jamii yetu haijaamuka katika michezo.
“Watu wafahamu kuwa michezo ni uchumi, uchumi unajengwa kutokana na michezo kwa hiyo watu wasidharau” amesema.
Mbio hizo zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni kilometa 21, kilometa 6 na kilometa 3 ambapo zinashirikisha watu mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu.
Mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 21 atazawadiwa tiketi ya Ndege kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Milan Italia kushiriki mchezo huo utakaofanyika Novemba 21 Mwaka huu utakaofanyika Milan.
Kwa upande wa wenye ulemavu, mshindi wa kwanza kwa kilometa 21 atapata shilingi laki tano (50,000/=).
Kwa upande wa kilometa 6, mshindi wa kwanza atapata shilingi laki tatu (300,00/=), mshindi wa pili atapata shilingi laki moja (100,000/=) na mshindi wa tatu atapata shilingi elfu hamsini (50,000/=).
Hali kadhalika mbio za kilometa 3 ambazo zitawashirikisha washiriki chini ya miaka 16, washindi watapewa vitabu mbalimbali vya shule.
Akitoa maelezo juu ya kushiriki Mwaisumbe alisema washiriki wamejaza fomu kulingana na umbali watakaoukimbia huku akiainisha kuwa fomu ya ushiriki kwa upande wa kilometa 21 gharama yake ni shilingi elfu ishirini (20,000/=), wakati kilometa 6 gaharama a fomu ni shilingi elfu kumi (10,000/=) na fomu ya kilometa 3 gharama yake ni shilingi elfu tano (5,000/=).
Ikiwa ni mwaka wa pili kwa Mkoa wa Iringa kufanyika mchezo wa Ruaha Marathon Mwaisumbe amesema wanatarajia kuwa na washiriki 400 tofauti na mwaka jana ambapo washiriki walikuwa 262.
Maandalizi ya Ruaha Marathon yamegharimu jumla ya shilingi 4,700,000/=.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment