![]() |
| Katibuwa wa chama cha wafanyakazi wa hifadhi, mahoteli, majumbani, huduma za jamii na ushauri Mkoa wa Iringa Mfumu Silvester akiongea na mtandao huu ofisini kwake. |
CHAMA cha wafanyakazi wa hifadhi,
mahoteli, majumbani, huduma za jamii na ushauri (CHODAWU) kimeanza mkakati wa
mikataba ya hali bora na mishahara kwa wanfanyakazi ili kuinua hali zao
kimaisha.
Akizungumza na mtandao huu
ofisini kwake leo Katibu wa chama hicho Mkoa wa Iringa Mfumu Silvester amesema
chama kimefikia uamuzi huo kutokana na hali ngumu ya maisha na kupanda kwa
gharama za maisha kutokana na mishahara yao kutokukidhi haja.
Amesema chma kinaanza kukutana na
waajiri kwa ajili ya kujadili na kusaini mikataba hiyo kwa ajili ya kuwawezesha
wafanyakazi wao kufanya kazi kwa moyo na kwa bidii.
“Kwa kuwa mikataba ya hali bora
ya wafanyakazi imeshaandaliwa, tunataka kukutana na waajiri ili tuweze kujadili
na kusaini ili ianze kutumika mara moja katika mwaka wa fedha na serikali
unaoanza Julai Mosi, Mwaka huu” amesema Mfumu.
Amesema Mkoa wa Iringa pekee una
taasisi nyingi ambazo ni wanachama wa chama cha wafanyakazi cha Chodawu ambao
wanalengwa kunufaika na mkataba huo.
Pia amesema taasisi hizo ni pamoja na
hifadhi kwa Camp Site zinazoshughulika na utalii ndani ya
hifadhi ya Ruaha ya Mkoa wa Iringa.
Ili kufanikisha hilo, amewataka wale wote ambao hawajajiunga
na Chodawu, wajiunge haraka ili wakati mikataba hiyo inaposainiwa waweze kujumuisha
kwa kuanza kunufaika nayo.
Amefafanua kuwa wanaohusika na
mkataba huo ni Hoteli zote, Lodge, Petro station, Super Market, Shule za
private, walinzi binafsi (security guard), Wafanyakazi wa Taasisi za dini (R.C,
K.K.K.T, Anglican) na waajiriwa wa ofisi za vyama vya siasa na taasisi za
huduma kwa jamii (NGOs).
“Kazi ya Chodawu ni kuhakikisha
kunakuwa na mahusiono na wajibu baina ya mfanyakazi na mwajiri inatekelezwa
inatekelezwa kulingana na sheria namba 6 ya ajira na mahusianao ya mwaka 2004”
amesema.
Chama cha wafanyakazi (Chodawu)
lianzishwa chini ya sheria ya usajili wa vyama vya wafanyakazi kifungu cha 8
cha sheria ya mwaka 1998.

No comments:
Post a Comment