![]() |
| Mtu ambaye jina halikuweza kufahamika mapema amenaswa akiwa katika usingizi baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni ulevi wa ulanzi. |
Ulanzi ni aina ya ya pombe yenye kilevi ambao upo kwa mfumo wa maji
na ina sukari yenye kumvuta mnywaji kuendelea kunywa.
Licha ya pombe hiyo kuwa n madhara,
watumiaji wengi wanajisahau na kujikuta wakishindwa kutembea kutokana na kunywa
kupita kiasi.
Pamoja na kuwa pombe hiyo huvutia
wanywaji kwa kiwango kikubwa, wapo baadhi ya watu ambao wanajikuta wakiahirisha
shughuli zao kwa sababu ya kunywa pombe.
Mtu mmoja ambaye jina lake
halikuweza kufahamika kwa haraka amekutwa na mtandao huu leo “akiuchapa”
usingizi kando ya barabara ya Dodoma Iringa katika kijiji cha Mgongo baada ya
kunywa ulanzi kijijini hapo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema mtu
huyo alifika kijijini hapo kwa lengo la kuhudhuria msibani lakini akakutana na
ulanzi ambao alikunywa kwa fujo kisha kusahau alichofuata.
“Mtu huyo hatumfahamu, alikuja
kwenye msiba lakini alipouona ulanzi akachanganyikiwa akaanza kuububuja. Lakini
hata hivyo inaonekana alikuwa hajala na ulanzi hautakiwi unapokunywa uwe na
njaa. Sasa angalia badala ya msiba amekuwa shida kwake tena” amesema shuhuda
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Kilwabulilo.
Hata hivyo ilikuwa ni vigumu kwa mtu
huyo kufanya chochote kwa kuwa amekuwa akiyumba huko na huko na kushindwa
kujificha katika kivuli jambo lililomsababisha kujianika kwenye jua.
Wataalamu mbalimbali wa vinywaji
vyenye kilevi (alcohol) wanasema hudhuru sehemu mbalimbali katika mwili wa
binadamu na kusababisha madhara makubwa na mabaya hasa utumiaji wa pombe
kali.
Wanasema sehemu kubwa zinazopata madhara
zaidi katika utumiaji wa pombe ni Ini kuharibika vibaya na kuwa kama kitu
kilichoungua kwa moto, Tumbo huweza kuchubuka hasa katika ngozi laini ya tumbo
la chakula na kusababisha vidonda vya tumbo.
Sehemu zingine ni Ubongo kuharibika
na kusababisha kupungua kwa kumbukumbu kumbukumbu, Mimba kuharibika na
kusababisha kuzaliwa kwa mtoto asiyekuwa na akili timamu (mtindio wa ubongo) pamoja
na kuleta madhara katika moyo na mapafu ya binadamu.

No comments:
Post a Comment