masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, March 11, 2013

MWENYEKITI WA KIJIJI AVULIWA MADARAKA NA WANAKIJIJI

Nape Nnauye


WANANCHI wa kijiji cha Madege kata ya Idete Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa wamemvua madaraka mwenyekiti wa kijiji hicho Philimino Msuva (CCM) kwa kile walichosema hawana imani naye kiutendaji na kiuajibikaji kwa ajili ya maendeleo ya kijiji hicho.

Msuva alizuliwa uenyekiti katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana kwa kupigiwa kura za kutokuwa na imani naye akishutumiwa kwa tuhuma mbalimbali za uawajibikaji.

Wakizungumza katika mkutano huo wananchi walionekana kuwa na jazba kutaka yeye mwenyewe ajiondoe katika meza kabla ya kupigiwa kura jambo ambalo hakulitekeleza na kuwafanya waanchi kulazimika kupiga za kutokuwa na imani naye.

Wananchi walidai kuwa mwenyekiti huyo tangu apewa dhamana hiyo, amekuwa hananguvu ya kiutendaji na kutumia madaraka vibaya huku akichekelea vitendo vya kishirikina hata pale vinapoonekana wazi bila kuchukua hatua.

Hata hivyo, imedaiwa kuwa tangu aingie madarakani hajawahi kusoma mapato na matumizi ya kijiji hata pale walipokuwa wakimtaka kutolea maelezo amekuwa hana majibu ya kuridhisha.

Kwamba kila ukiitishwa mkutano anapojitokeza mananchi kuuliza swali linalohusiana na mapato na matumizi, mwenyekiti huyo amekuwa akijibu kuwa mkutano ulioitishwa wa kutoa maagizo na maelezo kutoka ngazi ya juu na si wa kusoma mapato na matumizi huku akishindwa kuitisha mkutano wa kuwasomea wananchi mapato na matumizi.

Wananchi walisema, amekuwa akitumiwa familia yake katika masuala yanayohusu pesa huku akishindwa kutolea maelezo kwa wananchi ambao ndiyo watoaji wa michango na nguvu kazi ya kijiji.

Imeelezwa kuwa, pamoja na wananchi kutumia nguvu zao kukarabati nyumba za walimu, mwenyekiti huyo ameshindwa kuweka utaratibu unaofaa na kusababisha saruji iliyotolewa na wahisani kuganda bila kufanyiwa kazi.

Samabamba na hilo walisema matukio makubwa yanayotokea katika kijiji na kutakiwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi amekuwa akiyamaliza mwenyewe kwa rushwa huku akiwaacha wananchi wakiumia.

Wamesema kumekuwa na wananume wanaoumiza wake zao kwa kichapo lakini badala ya kuwachulia hatua za kisheria amekuwa akimalizana nao kwa rushwa na kuwaacha wanawake hao wakuhangaika na wakati mwingine wakihangaika bila kupata matibabu.

Tuhuma nyingine imeelezwa kuwa amekuwa akitumia jina la kijiji uiombea misaada familia yake huku akiacha wananchi wakihangaika kwa maendeleo yasiyosonga mbele kutokana na kile kinachochangwa kukibugia.

Wamesema amekuwa akitumia nguvu na vitisho katika kampuni ya Lung’ali (Maguta) kijijini hapo inayojishughulisha na nishati ya umeme ili kuwajaza watoto wake ambao wamekuwa wakiiba mali za kampuni hiyo bila kuchukuliwa hatua kwa kuwa baba yao amekuwa ndiyo mtetezi wao.

Hivi baribuni alipotea kijana mmoja Amuru Kiwone ambaye alifariki siku chache baada ya kupatikana katika mazingira ya kutatanisha huku mzee Limitel Mbombwe anayetuhumiwa kumchukua kijana huyo (marehemu) kishirikina akishindwa kuchukuliwa hatua za kisheria jambo lililowakera wananchi na kupandisha hasira za kumtaka mwenyekiti huyo kuacha kiti.

No comments:

Post a Comment