![]() |
| Hii siyo picha halisi |
MKAZI mmoja wa eneo la Bugarika jijini
Mwanza ameuawa na wananchi wenye hasira baada ya kufanya mauaji kwa
mwenzake kwa kumtenganisha kichwa, kisha kuanza kutamba nacho mtaani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza,
Ernest Mangu alisema tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa 7 na saa 8
mchana maeneo ya Bugarika.
Watu hao wawili waliokufa ni Bahati Vicent na Malimi Mathias ambao inadaiwa wakati wa uhai walikuwa karibu sana.
Akifafanua, Kamanda Mangu alisema watu
hao wawili walikuwa wanakunywa pombe katika kilabu ya pombe za kienyeji
wakati walipoanza kugombana wakidaiana fedha.
Alisema watu hao ambapo mmoja ni mmliki
wa kilabu hiyo walianza kudaiana fedha na baada ya kuzozana kwa muda,
Malimi alimkaba Bahati na kisha kumchinja na kumtenganisha kichwa na
kiwiliwili.
Kamanda huyo wa polisi alisema baada ya
kufanya mauaji hayo alianza kutembea mtaani na kichwa cha marehemu
Bahati na kuwaonesha watu ambao baada ya kuona unyama huo walipigiana
yowe na kujitokeza kwa wingi na kuanza kumshambulia Malimi hadi kufa.
Alisema Polisi walipofika katika eneo
hilo walikuta miili ya wawili hao na kuipeleka Hospitali ya Rufaa ya
Bugando. Alisema marehemu wanadaiwa kuwa marafiki wa karibu na kwamba
walikuwa mafundi wa ujenzi.
Akizungumzia Sikukuu ya Pasaka Mangu
alisema Polisi wamejipanga vyema kukabiliana na tishio la usalama kwenye
Makanisa na kutaka wananchi kusherehekea kwa amani.
Chanzo:bongo leaks

No comments:
Post a Comment