![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu |
MKAKATI uliopangwa na ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi wa kumng’oa ofisa kilimo wa Kata ya Itandula wilani
humo katika Mkoa wa Iringa ilishindikana baada ya mbinu walizozitumia kuonekana
ni za kupangwa.
Katika mkutano uliofanyika katani
hapo juzi ulilenga kuchafua na kung’oa ofisa kilimo Ngwalanje Emanuel kwa
tuhuma za kujihusisha na siasa kama mwanachama
wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya
hiyo Evarista Kalalu aliongozana na Ofisa utumishi wa Wilaya Denis Mselema, Afisa
Tarafa aliyetambulishwa kwa jina moja la Shirima, Diwani wa Kata ya Itandula Simon
Mangula na ofisa Mtendaji wa Kata Francis Ngano.
Hata hivyo mabalozi wa CCM alionekana
kila wakati kutafuta njia za kumtia hatiani ofisa kilimo hali iliojionesha wazi
wakizidiwa hoja na wananchi waliokuwepo katika mkutano huo waliokuwa wakipinga
vikali kuwa ni mbinu za kutengenezwa.
Mabalozi walionekana kumvaa ofisa
kilimo kila wakati ili kumtafutia makosa ni Enabu Nziku, Dickson Kaguo na
Brighton Mdendemi.
Kalalu alijiridhisha na majibu
yaliyojibiwa na ofisa huyo ambayo yalionesha kuwa tuhuma alizopewa ofisa huyo
ni za uongo.
Mabalozi hao walishindwa namna ya
kumtia hatianai kwa uongo jambo lililosababisha kuumbuka mbele za mamia ya watu
walijitokeza kupinga hoja zao za uongo ndipo ikamlazimu Mkuu wa wilaya kutumia
weledi wa kiuongozi baada ya kujiridhisha kuwa uongo umetumika kumtuhumu ofisa
huyo.
Katika hali ya kushangaza,
mabalozi hao walisikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya kutokutoa tamko la
kumfukuza ofisa huyo kazi na badala yake kuwataka viongozi wa umma kutumikia
jamii zao bila ubaguzi na kwa kujituma.
Mara baada ya mkutano huo
kufungwa chanzo cha habari kilichoomba jina lake
kutokuandikwa gazetini kilisema chanzo
cha mgogoro huo ni Chadema kuingia kwa akasi katika Kata hiyo jambo linalowapa
homa viongozi wa CCM kuanzia mabalozi katika chaguzi za serikali za mitaa
zinazokuja mbele yao .
“Unajua chanzo kikubwa cha
mgogoro huu ni kuingia kwa Chadema katika Kata hii kwa sababu viongozi wengi wa
CCM hadi sasa wana homa kupoteza viti vyao kuanzia katika chaguzi za serikali
za mitaa zitakazofanyika mwakani. Sisi hatuna tatizo na ofisa kilimo wetu kwa
kuwa ni mtu anayefanya kazi kwa upendo na kwa bidii bila kumbagua mtu yeyote,
siyo mtu wa rushwa wala mtu wa kuganganya. Yeye ni mkweli na ni mtu wa ushauri
na majadiliano” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilisema tuhuma
alizobebeshwa ofisa huyo zilipagwa siku moja kabla ya mkutano uliofanyika na
baadhi ya viongozi wa chama cha Mapinduzi na kujipanga namna ya kuwasilisha
uongo huo mbele ya Mkuu wa Wilaya.
“Kabla ya kikao walichokaa siku
moja kabla ya Mkutano mimi nikiwa miongoni kusikiliza kinachopagwa juu ya ofisa
wetu, viongozi hao waliandika barua kwa Mkuu wa Wilaya juu ya tuhuma hizo. Ili
kuonesha nguvu ya tuhuma zao ndipo walipokaa na kujipanga namna ya kutetea hoja
zao lakini kama ulivyojionea mwenyewe
wameshindwa. Kitu cha uongo daima hakina nguvu” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilionesha ushahidi
wa sauti zilizo naswa katika kikao hicho kilichodaiwa kililenga kupanga mbinu
ya kumchafua na kumtia hatiani ofisa kilimo ili ang’olewe katika nafasi yake.
Hata hivyo imeelezwa kuwa mbinu
hiyo itaendelea kufanyika maeneo mengine ikiwamo ya kuwabambika kesi wanachama
na wafuasi wa Chadema ili kudhoofisha kasi ya upinzani vijijini.
Wakati mkutano huo ukifungwa Mkuu
wa Wilaya aliwataka wananchi kuwaheshimu wataalamu wao ili kuweza kupata ujuzi
na utaalam katika utendaji wa shughuli zao na kuachana na mizengwe isiyokuwa na
tija katika maendeleo.

No comments:
Post a Comment