masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, February 18, 2013

Kinana ni mtuhumiwa wa ujangili

Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa akiwahutuba wakazi wa Manispaa ya Iringa katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika maeneo ya Soko Kuu mkabala na Kituo Kikuu cha Polisi.


MBUNGE wa Iringa mjini Peter Msigwa (CHADEMA) amesema dhamira yake ya kupeleka hoja yake binafsi bungeni juu ya ujangili wa tembo bado ipo pale pale pamoja na kuwa katika vikao vya bunge lililopita hakupewa nafasi.

Mch. Msigwa aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika maeneo ya Soko Kuu mkabala na kituo Kikuu cha Polisi katika Manispaa ya Iringa.

Alisema pembe za ndovu zinazokamatwa katika kila kona ya dunia zinatoka Tanzania jambo linalotishia usalama wa wanyama katika mbuza za Taifa.

Kutokana na ujangili huo Msigwa ambaye pia ni Waziri kivuli wa maliasili amemtaja Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdalah Kinana kuwa ni miongoni mwa watuhumiwa wa pembe za ndovu nchini.

“Wahusika wakubwa ni baadhi ya polisi na usalama wa taifa wasiowaadilifu ambao wanajihusisha na wizi wa pembe za ndovu” alisema.

Alisema viongozi wengi wa ngazi ya juu katika chama cha Mapinduzi ambao leo wanajinadi kwa wananchi kuonekana wasafi ni miongoni mwa majandili na wizia wa pembe za ndovu.

“Leo hii mtu unajiita Mnec wakati kipindi cha baba wa Taifa alikuwa ni mtuhumiwa wa pembe za ndovu! Pia nawashangaa watu wa usalama wa taifa, mnang’ang’ania kunasa sauti yangu katika mikutano wakati Twiga na tembo huko wanauawa. Ni usalama gani huu?” alisema  na kuhoji Msigwa.

Hata hivyo alisema zinapojitokeza hoja za msingi ambazo ni manufaa kwa umma na kufunikwa ni wazi kuwa wapo baadhi ya watu ambao wamezoea uongo badala ya ukweli na kwamba kilichotokea katika vikao vya bunge lililopita ni ukiukwaji wa makusudi wa taratibu za nchi.

“Leo hii vyombo vinavyotakiwa kulinda maadili, ndivyo hivyo hivyo vinavyotumika kuhujumu nchi. Kama mlivyoona hoja zenu wananchi zikizimwa kule bungeni, tulichokifanya ni mwanzo ila kama hali hii itaendelea, kipo kinachokuja ambacho ni kikubwa kuliko kile. Tunapotetea huduma za jamii wanatuambia tunafanya fujo. Ni wenda wazimu gani huo?” alisema.

Katika hatua nyingine Msigwa alisema vurugu na mauaji mbalimbali yanayotokea nchini kuhusishwa na imani za kidini ni mpango wa kisiasa ambao wanasiasa wa chama cha Mapinduzi wanautumia ili kuwagonganisha wanchi kidini.

“Kila wakati tunasikia mauaji na vurugu za kidini, mtakumbuka juzi kuna mchungaji amechinjwa kule Geita na leo Padri wa Kanisa Katoliki amepigwa risasi huko Zanzibar. Huu ni mpango wa CCM kutugonganisha kidini kwa kuwa kila wanachokifanya kinagonga mwamba. Miaka 50 tumeishi kwa kuheshimiana bila vurugu za kijinga kama hizi lakini iweje leo katika utawala wa Kikwete uibuke udini? Huo ndio mpango wake na yeye akiwa mhamasishaji mkubwa wa udini ili kutugonganisha” alisema.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi (CHADEMA) alisema matatizo mengi yanayojitokeza nchini yanasababishwa na udhaifu wa serikali iliyochoka.

“Watu wavamia maeneo kwa sababu ya mipango mibovu ya serikali iliyopo madarakani, kuenda kwenye huduma za afya hakuna dawa, basi wabinafsishe hospitali hizo ili tujue moja!, vituo vya polisi vinaendesha doria kwa kuomba fedha kwa watu binafsi ili wanunue mafuta. Wakiwaomba ninyi wananchi kama mnazo wapeni kwa sababu serikali imeshindwa kuwahudumia” alisema Nyalusi.

Naye Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Arusha Dadi Igogo alisema kutokana na kauli za CCM kutaka kukomboa majimbo, wananchi wanatakiwa kuwa makini na kauli hizo kwa kuwa hazina mantiki yoyote katika maisha.

“Kwa miaka 50 tulikuwa na maadui watatu ambao tulikuwa tukiwapiga vita ambao ni ujinga, Umasikini na Maradhi lakini sasa hivi ameongezeka adui mwingine ambaye ni mbaya sana anaitwa CCM. Ndugu zangu kuweni makini na adui huyo atatumaliza” alisema Igogo.

Alisema moja ya kauli ambazo zinaonesha dhahiri kuwa CCM ni chama cha watu wasio na nidhamu, ni kauli za Nape Nnauye ambazo daima yeye ni matusi hata kuwatukana wazazi wake.

“Naomba kumuuliza Nape, ina maana upevu wake wa nidhamu umeanzia kwa Dkt. Slaa? Kama hawezi kumheshimu Dkt. Slaa, kwani nini hajamwambia baba yake kuwa ni mtoto wake? Sasa CCM wanapojiandaa kukomboa jimbo, Msigwa anaendelea kuwakomboa watu wa Iringa. Wamsiwasikilize waliofilisika kufikiri na kuwajibika watawatupa motoni” alisema.

No comments:

Post a Comment