![]() |
| Mlipano Henry akirudisha kadi ya CCM kawa Katibu wa Chadema tawi la Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa. |
![]() |
| Mlipano Henry akipokea kadi ya Chadema mara baada ya kurudisha kadi ya CCM. |
![]() |
| Katikati mwenye mavazi meusi ni Mlipano Henry akikabidhiwa skafu ya Chadema kama kitambulicho cha chama. |
![]() |
| Mlipano Henry akivikwa skafu ya Chadema tayari kwa kuanza kukitangaza chama. |
KADA maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mlipano
Henry amerudisha kadi ya chama chake na kuhamia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) katika tawi la Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa.
Akizungumza wakati akirudisha kadi hiyo jana Mlipano
ambaye pia ni Waziri wa Michezo katika serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa alisema amefikia uamuzi huo kutokana na dhuruma na uonevu aliouona katika chama
chake.
Alisema amefanya maamuzi magumu baada ya kubaini
kuwa alipotea tangu mwanzo kwa kuwa hakuwa na uelewa wa kutosha juu ya uzalendo
wan chi na uungwana kwa Watanzania wenzake.
“Nimefikiri sana kuchua maamuzi haya lakini baada ya
kuona nchi hii inakoelekea ni kubaya nikaamua kwa dhati kutoka rohoni kuachana
na CCM kwa kuwa chama hicho kinalipeleka taifa pabaya” alisema Mlipano.
Miongoni mwa sababu alizotoa kukihama chama cha
mapinduzi alisema ni mpasuko mkubwa uliopo ndani ya chama na kwamba kila mtu
anataka kutumia madaraka yake kwa malahi binafsi huku akijua kuwa anaiba mali
ya umma.
“Chama chetu hakina ushirikiano kiasi cha kujificha
hata ninapotembea, mfumo wa serikali yangu iliyopo madarakani nimeona si mzuri
bali unaleta machungu kwa wananchi na kama utaendelea hivi kutakuwa na hali
mbaya sana siku za usoni.
Kwamba, nimesikitika sana matokeo ya kidato cha nne.
Huu ni mfumo wa serikali yetu na si vichwa vya wanafunzi, hata mpasuko wa
kiimani unaoendelea unanisikitisha sana kuona serikali yangu iliyopo madarakali
inaangalia tu. Serikali inaliona lakini viongozi wanapuuzia” alisema.
Hata hivyo alisema umasikini uliokithili kuliko
maelezo unatokana na mfumo mbovu wa serikali iliyopo madarakani kwani viongozi
wengi hawana uwezo wa kufikiri na badala yake wanaangalia matumbo yao tu.
Mtandao huu umefanikiwa kuupata ujumbe wa Mlipano kupitia
simu ya mkononi alioutuma kwa viongozi wake kuiaga CCM na kuhamia Chadema.
Ujumbe huo unasomeka “kwa heshima na taadhima,
nakujulisha rasmi kuwa narudisha rasmi kadi ya CCM na nahamia CHADEMA. Nimefikia
maamuzi haya nikiwa timamu na kamili. Sipo tayari kushuhudia uonevu na chuki
inayoendelea ndani ya chama. Nawatgakieni kila la kheri ila hakika nitahamishia
nguvu zote Chadema na nitawapa ushirikiano wote. Naungana na waangwana kutafuta
tone la mwisho la damu ya waasisi wa faifa la Tanzania”.
Hata hivyo majibu ya ujumbe huo yalipatikana kwa
njia ya ujumbe mfupi kupitia simu ya kiganjani ukisomeka “nenda salama na
nakutakia siasa njema huko Chadema. CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa tofauti
ni kwamba CCM ni chama tawala na CDM ni chama Kikuu cha upinzani”.
Joseph Mtama mwanafunzi wa chuo hicho akishuhudia
kurudishwa kwa kadi hiyo alisema kama kuna dhambi kubwa, ni dhambi ya
unafiki na kumtaka Mlipano
kutokujitumbukiza katika dhambi hiyo kwa kuwahadaa wanachi.
“Kiongozi yoyote anayetgambua haki za binadamu, na
anafaa kuigwa . lakini ndugu yangu, kutetereka kwa kiongozi mmoja , ni udhaifu
wa mtu binafsi. Unapoyaona hayo wewe simama imara na kusonga mbele. Unapomuona kiongozi
mmoja anayumba, watu huwaangalia waliowengi na kuwafuata. Uwe mfano wa kiongozi
imara usiyumbe” alisema Mtama.
Naye Marere Nyamsi mjumbe wa baraza la wazee
Chadema, alisema ushirikiano ni nyenzo ya kuleta matunda mazuri nay a maendeleo.
“Sisi tunafanya kazi kwa kushirikiana na kunyeshewa
na mvua kwa sababu tunajua ni haki ya watu kupata elimu inayostahili. Usikate tamaa,
songa mbele. Tuna imani hutaogopa chachote” alisema.
![]() |
| Miongoni mwa kadi za CCM zilizorudishwa katika tawi la Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa. |
![]() |
| Mlipano Henry aliyekaa katikati akiwa na baadhi ya wanachuo walioshuhudia akirudisha kadi ya CCM na kujiunga na Chadema. |






No comments:
Post a Comment