masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, January 28, 2013

WAKULIMA WAASWA KUZINGATIA MAFUNZO YA KITAALAM.

WAZIRI wa fedha na uchumi William Mgimwa akiwa ofisi za wataalam  kupitia mradi  wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) mkoani Iringa akizungumz na watekelezaji wa mradi huo pamoja na  wakulima  wa mazao ya nyanya na alizeti hivi karibuni.


KATIBU wa shirikisho la wakulima
  wa nyanya na mali mbichi, Magnus Kimbe akisoma risala kwa niaba ya wenzake mbele ya Waziri Mgimwa katika ofisi za MUVI zilizopo mkoani Iringa hivi karibu baada ya kutembelea na Waziri huyo kuongea nao.


WAKULIMA wametakiwa kufuata ushauri wa wataalam wanaojitolea kutoa mafunzo kwa wakulima mbalimbali ili kukiwezesha kilimo kuwa bara na chenye manufaa kwa kwa taifa.

Ushauri huo ulitolewa hivi karibuni na Waziri wa fedha na uchumi William Mgimwa alipotembelea ofisi za wataalam  kupitia mradi  wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) mkoani Iringa kuzungumza na watekelezaji wa mradi huo pamoja na  wakulima  wa mazao ya nyanya na alizeti.

Mgimwa alisema  nchi nyingi zilizowekeza katika mafunzo  na wakaazi wake wayakazingatia ndizo zilizofanikiwa zaidi duniani.

“Nchi nyingi  zilizowekeza katika mafunzo ndizo zilizofanikiwa zaidi Duniani,ukienda China waliwekeza zaidi katika mafunzo na wamepiga hatua kiuchumi, zingatieni haya mafunzo mnayopatiwa na wataalam kutoka mradi wa MUVI” alisema Mgimwa.

Wakulima waliwaasa kufanya kwa vitendo yale yote wanayofundishwa na wataalam ili waweze kufanikiwa  katika kile wanachozalisha.

Ikumbukwe kuwa katika utekelezaji wa kilimo kama ilivyo katika kaulimbiu ya “kilimo kwanza” serikali ndiyo yenye jukumu la kusimamia kwa vitendo lakini wanapojitokeza wadau mbalimbali kusimamia huongeza ufanisi kama ilivyo kwa utekelezaji wa mradi wa MUVI.

Serikali inapaswa kutambua mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali hasa yale yanayofanya kazi ambazo serikali ilipaswa kuwajibika moja kwa moja kwani ushirikiano huo unaonesha kuleta babadiliko ya kimaendeleo.

Mradi wa MUVI umefanikiwa kuwaunganisha wakulima katika vikundi mbalimbali katika Mikoa ya Iringa na Njombe ili kuwawezesha kuboresha kilimo chao kwa ajili ya kuongeza pato lao na la taif kwa ujumla.

Licha ya juhudi za mradi huo kushika kasi, serikali ambayo ndiyo yenye jukumu la utekelezaji wa kauli mbiu ya kilimo kwanza imelalamikiwa kutotekeleza kwa vitendo jambo ambalo bado linaonesha utekelezaji wa maneo bila vitendo.

Hivi karibuni wananchi mbalimbali kutoka katika Halmashauri ya Iringa wametoa malalamiko yao kuwa serikali haiwajibiki ipasavyo kutokana na upatikanaji wa pembe jeo kuwa mgumu licha ya serikali kuimba wimbo wa kilimo kwanza.

Halmashauri ya iringa ambayo ina vikundi vingi vilivyoundwa na mradi wa MUVI pembejeo imekuwa ni kitu cha nadra kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuna mpango mzuri wa ugawaji wa ruzuku hiyo.

Wakulima mbalimbali walitoa maoni yao kuwa hakuna haja ya kuzungumzia masuala ya pembejeo wakati upatikanaji wake unakuwa mgumu na hata zikipatikana gharama yake haifikiwi kiurahisi.

Mradi wa MUVI unaonesha matumaini kwa wakulima kutokana na wengi ambao wako kwenye vikundi kuonesha mafanikio ya maendeleo ya kilimo bora.

Mradi wa MUVI unatekelezwa kwa mfumo wa  dhana ya mnyororo wa  ongezeko la thamani kwa upande wa zao la nyanya na alizeti mkoani Iringa.

Licha ya serikali kulalamikiwa kwa ukosefu wa pembejeo, Wazili Mgimwa, ameendelea na ahadi za mkopo kwa wakulima wanaozingatia yale yote yanayopaswa katika kufanikisha kilimo bora hasa kufuata ushauri wa wataalamu mbalimbali hasa MUVI.

Alisema mkulima anayefanya  vizuri katika shughuli yake  anakopesheka ili alime kitaalam na   azingatia kanuni za kilimo  bora hapo anaweza kukopesheka.

“Hakuna asiyekopesheka, kila mtu anayejishughulisha na  shughuli yeyote halali inayeonekana anasifa za kupata  mkopo  kutoka kwenye taasisi  mbalimbali za kifedha, ila  mkopaji lazima aoneshe jitahada na ufanisi wa hali yajuu utakaomridhisha mkopeshaji; tatizo wakulima wengingi wanalima bila kuzingatia kanuni za kilimo bora, hawapandi kitaalam, hawatumii mbolea na wala hawazingatii kile wanachofanya halafu wanasema hawakopesheki, hakuna  benki au mtu binafsi anayeweza kukopesha  mkulima  wa aina hiyo” alisema.

Wakulima wa nyanya na alizeti  wilaya za Iringa, Kilolo na Njombe wana bahati kubwa kwa kuwepo kwa Mradi wa MUVI unaojihusisha na kuongeza thamani katika mazao hayo ambapo wamekuwa wakipata mafunzo ya kilimo bora, elimu ya ujasiriamali, elimu ya  biashara na  mawasiliano pamoja na elimu ya  namna ya kuandaa mpango biashara na  sifa za kukopesheka.

Kilimo ni sekta  kubwa inayopaswa kuheshimiwa kwa kuwa  Taifa na mtu mmoja mmoja wanategemea kilimo ili waweze kujikimu kimaisha sanjari na kupambana na baa la njaa.

Awali Katibu wa shirikisho la wakulima  wa nyanya na mali mbichi, Magnus Kimbe akisoma risala kwa niaba ya wenzake, pamoja na mambo mengine alimuomba Wazir Mgimwa kuwa msimamizi wa shirikisho lao ili waweze kuwa na mshikamano.

Hata hivyo Mgimwa aliwataka kufanya marekebisho ya katiba yao ili kuingiza kipengele hicho ili awe tayari kushirikiana nao kwa pale watakapomhitaji.

No comments:

Post a Comment