Umoja wa wanafuzi wa vyuo
vikukuu katika Manispaa ya Iringa wameendele na zoezi la kufanya usafi katika
Manispaa kama moja ya ushiriki wao katika masuala ya kijamii.
Licha ya kuonesha umoja
wao katika maeneo mbalimbali bado muamko wa viongozi wa mitaa pamoja na madiwani
wa kata husika wameonekana kutopendezwa na na masuala hayo kwa kile
kinachoonekana kutoshiriki na kuahamasicha wananchi kuungana na watu
mbalimbali.
Rose Mayemba ambaye ni
mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika tawi la Chuo
Kikuu cha Ruaha (RUCO) mlipuko wa magonjwa mbalimbali hauchagui itikadi za
vyama na waathirika ni mtu yo yote bila kujali cheo na chama chake.
“Suala usafi linamlenga
kila mtu bila kujali itikadi za siasa. Magonjwa yanapotokea hayawezi kuchagua
siasa au itikadi. Watu wanaoingiza itikadi ya vyama katika masuala ya afya wana
mawazo fivyu” alisema.
Halmashari ya Iringa
inapaswa kuangalia upya na kuzuia ujenzi holela wa nyumba ili kuhakikisha
mazingira yanakuwa safi na kuendeleza utamaduni wa kuhifadhi mazingira.
“Halmashaur inatakiwa
kuzuia ujenzi holela katika maeneo ya milima na badala yake maeneo hayo
yapandwe miti. Mimi ningefikiri sehemu za milimani tungepanda miti ili
kuendeleza mpango wa taifa kuhifadhi mazingira ili kulinga hali ya hewa kuwa
safi lakini tunapojenga huko tunaendelea kuyaharibu” alisema.
Vitus Rupeche
mwanafunzi wa Chuo Kikuu kishiriki cha Tumaini alisema watu wanaojiita wasomi
na kuishi sehemu chafu ni kuidharirisha elimu.
“Wasomi hawawezi kuishi
sehemu chafu. Hivyo sisi wanafunzi tunatambua kuwa tupo katika jamii kwahi
tunaungana na jamii katika masuala ya ufasi kwa sababu ni jukumu letu
kuhamasisha” alisema Rupeche.
Hata hivyo ameonesha
masikitiko yake kuona viongozi wa mitaa pamoja na madiwani wa sehemu husika
hawana muamko wa kushirikiana na wadau mbalimbali wa usafi katika kuyaweka
mazingira yao safi.
“Kinachonisikitisha
hapa ni pale ninapoona viongozi wa maeneo husika hawaoini umuhimu wa ufasi
katika maeneo haya. Tutaendelea na itikadio zetu mpaka lini katika masuala haya
ya kijamii? Inasikitisha sana” alisema na kuhoji.
Wakati huo huo Hilda
Mbinda mwanafunzi wa RUCO alisema kushiri kwa viongozi hao ni kushindwa
kufikiri na kujua maana ya usafi.
“Nitaendelea
kuwashangaa hawa wanaoitwa viongozi. Kushindwa kushiriki katika masuala kama
haya kunaonesha ni jinsi gani hawana fikra na kutoelewa maana ya usafi”
alisema.
Naye Olime Mwakilembe
alisema vijana wana uwezo mkubwa katika maendeleo na hivyo kuwataka wasiwe
nyuma kutumia nguvu katika kupiga hatua za kimaendeleo.
“Sisi vijana tunaweza
ndiyo maana tumeamua kutumia nguvu zetu katika masuala. Vijana tunaomba
tushirikiane kwa pamoja katika ujenzi wa taifa letu. Tusikubali kuvutwa na watu
wasiopenda maendeleo eti kwa itikadi za vyama” alisema Mwakilembe.
Wanafunzi hao walianza
kwa kupanda miti katika maeneo ya viwanja vya bustani ya Manispaa maarufu kwa
jina la (garden) na baadaye kufanya usafi katika maeneo ya makaburi ya
Mlandege.
No comments:
Post a Comment