![]() |
|
Jeshi
latumia vifaru kuwafurusha waandamanaji kutoka Tahrir.
|
Wanajeshi
nchini Misri wameanza kuwaondoa watu kutoka katika eneo la ikulu ya rais mjini
Cairo ambako kumekuwa na makabliano makali kati ya wafuasi na wapinzani wa rais
Mohammed Morsi
Limetuma
vifaru na magari mengine yaliyo hamiwa kwa silaha nje ya kasri la rais baada ya
mapigano ya usiku kucha kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi.
Walioshuhudia
matukio wanasema kuwa waandamanaji wameanza kuondoka kutoka eneo hilo.
Makabiliano
yamesababisha vifo vya watu watano na wengine zaidi ya mia sita wakijeruhiwa.
Taarifa
za televisheini ya taifa zinasema kuwa rais Morsi atatoa hutuba kwa taifa
baadaye leo.
Mamlaka
kuu ya waisilamu, Al-Azhar,imemtaka rais kufutilia mbali mamlaka
aliyojilimbikizia.
Viongozi
wa upinzani wameitisha maandamano zaidi hii leo kupinga hatua ya rais kujipa
mamlaka zaidi pamoja na kuipinga rasimu ya katiba mpya inayotarajiwa kupigiwa
kura tarehe 15 mwezi huu.
Pande
hizo mbili zilitumia mawe, na mabomu ya petroli kushambuliana baada ya wafuasi
wa rais kujaribu kulitawanya kundi la upinzani lililokuwa likiandamana nje ya
kasri la rais.
Upinzani
umeshutumu chama cha Muslim Brotherhood kupanga mashambulio hilo Vurugu hizo
zilisambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo huku ofisi za Muslim Brotherhood
zikishambulia katika miji ya Ismailia na Suez.
Washauri
wanne wa rais Morsi wamejiuzulu.
Upinzani
unasema upo tayari kwa mazungumzo iwapo Morsi atasitisha agizo linalompa
mamlaka mpaya ya zaidi na iwapo ataahirisha kura ya maoni ya kielelezo cha
katiba.

No comments:
Post a Comment