| Asko wa Jimbo la Iringa Mhashamu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa akiweka shada juu ya kaburi la marehemu Pd. Massawe. |
| Asko wa Jimbo la Singida Mhashamu Desderius Rwoma akiweka shada juu ya kaburi la marehemu Pd. Massawe. |
| Asko wa Jimbo la Njombe Mhashamu Alfred Maluma akiweka shada juu ya kaburi la marehemu Pd. Massawe. |
| Asko wa Jimbo la Mbeya Mhashamu Evaristo Chengula akiweka shada juu ya kaburi la marehemu Pd. Massawe. |
| Kaka wa Marehemu Pd. Massawe akiweka shada juu ya Kaburi. |
| Mama wa marehemu Pd. Massawe Maria Illuminata akiweka shada juu ya kaburi la mwanawe. |
| Sr. Pascalina Mkolomi wa Consolata akiweka shada juu ya kaburi akisaidiwa na Mhashamu askofi Ngalalekumtwa. |
| Add caption |
| Wanafamilia ya Pd. Massawe wakiwa mbele ya kaburi baada ya mazishi. |
| Wanafamilia ya Pd. Massawe wakiwa mbele ya kaburi. |
| Wanafamilia wakiwa mbele ya kaburi. |
Padre Salutaris Lello Massawe
alizikwa kichifu kwa kupigiwa mizinga hewani kutambua uwajibikaji enzi za uhai
wake.
Pd. Massawe ameitwa na Mungu
wakati ambao shirika lilikuwa bado linamhitaji kwa ajili ya uwajibikaji wake
hasa katika kulitumikia shirika, Mungu na kuchunga kondoo wa Bwana
aliokabidhiwa.
Bado ni kama ndoto kwa waamini
hasa jimboni Iringa ambako makao makuu ya shirika la Consolata Tanzania yapo
japo kuwa hawana budi kuyapokea mapenzi ya Bwana aliye muumbaji.
Padre Salutaris Lukas Massawe
Lello alizaliwa Moshi Julai 8, 1962. Baba yake ni Lukas Victor na Mama, Maria
Illuminata Manka.
Alisoma katika shule ya msingi ya
Singachini kati mwka 1971 – 1978, akajiunga katika seminari ya Maua ambapo alisoma mpaka
1985, alipohitimu masomo ya sekondari.
Mwaka 1985 alianza masomo ya
falsafa na teolojia katika seminari ya Consolata ya Nairobi na kuhitimu mwaka 1988 alipoanza
unovisi. Alimaliza unovisi mwaka 1989 na akafunga nadhiri za kwanza 21 Julai
1989 Sagana (Kenya).
23 Oktoba 1992 alifunga nadhiri
za milele Nairobi
na 28 Novemba 1992 akapewa daraja la ushemasi.
Julai 27, 1993 alipewa daraja la
upadre Moshi kwa kuwekewa mikono na Mhashamu Baba Askofu A. Msarika.
Pd. Massawe alifanya kazi ya
umisionari katika nchi ya Ethiopia
kutoaka 1995 hadi mwaka 2000 baada ya hapo akatumwa Italia akifanya kazi ya
uhamasishaji wa roho ya umisionari hadi mwaka 2007 aliporudi Tanzania.
Baada ya kusoma katika Chuo Kikuu
cha Mt. Augustino Mwanza, akatumwa Bunju, Dar
es Salaam kwa ajili ya shughuli za gazeti la
wamisionari wa Consolata “Enendeni. Kutoka Septemba 7, 2011 alikuwa Baba Mkuu
wa Shirika la Wamisionari wa Consolata nchini Tanzania.
Pd. Massawe alifariki Oktoba 25,
2012 Bagamoyo kwa ajali ya Maji na kuzikwa Oktoba 30, 2012 katika makaburi ya Jimbo
yaliyopo Tosamaganga.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa serikali na madhehebu ya kidini kutoka ndani na nje ya
nchi ambapo jumla maaskofu wanne walihudhuria mazishi hayo.
Maaskofu hao ni pamoja na
Mhashamu Desderius Rwoma wa Jimbo Katoliki la Singida, Mhashamu Alfred Maluma
wa Njombe, Mhashamu Evaristo Chengula wa Mbeya pamoja na Mhashamu Tarcisius
Ngalalekumtwa wa Iringa ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania.
Mungu aiweke roho yake mahala
pema ……. Amina
Hapa ndipo tunakomea kwa matukio ya Mazishi ya Pd. Salutaris Lelllo Massawe. Mungu akubariki kwa kufuatilia matukio haya mpaka mwisho. Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.
No comments:
Post a Comment