masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, November 24, 2012

NZIGILWA MLINZI WA KANISA KATOLIKI KIHESA ALIYEJERUHIWA NA MAJAMBAZI AAGA DUNIA

Damu ya marehemu Bathlomeo Nzigilwa ilivyotiririka baada ya kuvamiwa na majambavi na kujeruhiwa vibaya akiwa kazini.

Bathlomeo Nzigilwa alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Iringa kabla ya kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili.
Mlinzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kihesa Jimbo la Iringa Bathlomeo Nzigilwa aliyejeruhiwa vibaaya baada ya kuvamiwa na majambazi usiku wa kuamkia Novemba 15 mwaka huu amefariki dunia leo dakika chahe zilizopita.

Nzigilwa amefariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili alikopelekwa kwa matibabu baada ya kuondolewa katika hospitali ya Mkoa wa Iringa alikokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa.

Uvamii uliofanyika kanisani hapo ulikenda sambamba na uharibifu wa mali za Kanisa vikiwemo vyombo vitakatifu vya ibada.
 
Mavazi ya ibada na vifaa mbalimbali vya ibada viliharibiwa vibaya, Taberenakulo ndogo nayo ikiharibiwa, msalaba kuvunjwa pamoja na Hostia Takatifu zikimwagwa kila mahali pamoja na fedha kadhaa kuibwa..
Utaratibu wa mazishi utaelezwa kadiri ya mipango itakavyokuwa inaendelea kupangwa.



Bwana ametoa na Bwana ametwa, jina la Bwana lihimidiwe.

Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema mbinguni .... Amina.

No comments:

Post a Comment