masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, November 7, 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI HAKUFIKISHWA MAHAKAMANI

MTUHUMIWA wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi aliyetakiwa kufikishwa mahakamani leo hakufikishwa kutokana na sababu iliyoelezwa kuwa gari la kubebea mahabusu halikuwa na mafuta.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya Dyness Lyimo amesema Pasificus Cleophace Simon (23) mtuhumiwa wa mauaji ya mwandishi huyo pamoja na watuhumiwa wengine waliopo mahabusu hawakufikishwa mahakamani kwa sababu ya gari linalotumika kuwapeleka mahakamani hapo halikuwa na mafuta.

"Tatizo kubwa lilopo sasa hivi ni uhaba wa mafuta kwa sababu hata mimi mwenyewe gari langu halina mafuta; sisi mafuta tunategemea mafuta kutoka boharini na kwa bahati mbaya bohari haina mafuta" amesema.

Hata hivyo Lyimo amesema kuwa kulikuwa na uwezekano wa kumpeleka mtuhumiwa huyo wa mauaji ya mwandishi kwa kumsindikiza kwa miguu kutokana na gereza kuwa jirani na mahakama lakini hawakufanya hivyo ili kuzuia kuteka hisia za watu ambazo zingeweza kusababisha fujo.

"Kulikuwa na uwezekano mkubwa wa watuhumiwa kuletwa mahakamani kwa miguu lakini haikuwezekana kwa sababu askari wasingeza kumchukua mtuhumiwa mmoja na kuwaacha wengine ambao walipaswas kusomewa mashtaka yao hapo jana" amesema.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo mwenye namba G 2573 kila anapofikishwa mahakamani, hufikishwa kwa gari la peke yake ambapo kwa awamu iliyopita alifikishwa kwa gari la polisi lenye namba PT 1467 likiwa na ulinzi mkali.

Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani hapo kwa gari namba DFP 2175 pick up akiwa katika ulinzi mkali.

Kwa mujibu wa hakimu huyo, kesi imeahirishwa hadi Novemba 21 mwaka huu itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment