![]() |
Mauti hayo yamemkuta leo majira ya saa 5 asubuhi katika hospitali hiyo wakati madaktari na wauguzi mbalimbali walipokuwa wakifanya juhudi za kuiokoa uhai wake
Mhashamu Askofu Aloysius Balina alizaliwa Juni 21, 1945 katika
kijiji cha Isoso Ntuzu wilayani Bariadi mkoani Shinyanga akwekwa
wakfu na Papa Yohane Paulo II mwaka 1984 kuwa Askofu wa Geita na
kusimikwa Machi 10, 1985.
Septemba 23, 1997 alihamishiwa Jimbo la Shinyanga na kuwa Askofu wa
tatu wa Jimbo la Shinyanga hadi mauti yalipomkuta, huku watangulizi
wake wakiwa Askofu Edward A. Mc Gurkin, aliyetumikia cheo hicho toka
mwaka 1956 hadi 1975, alifariki Agosti 28, 1983 huko Marekani, wa pili
ni Askofu Castor Sekwa, aliyetumikiwa kuanzia mwaka 1975 hadi Juzi 6,
1996 alipofariki na askofu Balina kushika nafasi yake.
Mpango wa wazishi unaendelea kufanyika na taarifa zaidi tutaendea kupata.
Mungu aiweke roho yake mahala pema ............ Amina.

No comments:
Post a Comment