masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, October 24, 2012

Mtuhuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi afikishwa mahakamani kwa mara nyingine

Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa kituo cha Runinga cha Channel Ten katikati aliyevaa jaketi jeupe akifikishwa mahakamani leo.

Aliyejifunika kofia ya jaketi jeupe ni mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha runinga cha Channel Ten alipokuwa mahakamani leo.

MTUHUMIWA wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi amefikishwa mahakamani leo katika ulinzi mkali huku waandishi wa habari wakizuiwa kupiga picha.

Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia wengine wakiwa na virungu, silaha za moto huku wengine wakivaa kiraia walitandaa mahakamani hapo kuhakikisha waandishi wa habari hawapati mwanya wa kupiga picha.

Wakili wa serikali ambaye pia aliendesha mashtaka ya mtuhumiwa huyo Lilian Ngilangwa aliambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Dyness Lyimo kuwa upelelezia wa kesi hiyo haujakamilia.

Pasificus Cleophace Simon (23) alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tuhuma ya kumuua kwa makusudi mwandishi huyo katika ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa uliofanyika Septemba 2 mwaka huu.
  
Mtuhumiwa huyo mwenye namba G 2573 alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la polisi lenye namba PT 1467 likiwa na ulinzi mkali.

Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO  huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani hapo kwa gari namba DFP 2175 pic up akiwa katika ulinzi mkali huku waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika kupigwa jambo lililozusha hisia tofauti miongoni mwa wananchi wengi mkoani hapa.

Kwa mujibu wa wakili huyo, upelelezi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Novemba 07 mwaka huu itakapotajwa tena.

Wakati waandishi wahabari wakiwajibika mahakamani hapo kutafuta uwezekano wa kumpiga mtuhumiwa huyo picha, mwandhishi wa habari wa gazeti Majira Eliasa Ally amepigwa na askari akizuiliwa kupiga picha.

Askari aliyempiga mwandishi huyo ametambuliwa kwa jina moja la Idirisa jambo ambalo limezua hisia mbalimbali miongoni mwa waandishi hao pamoja na wananchi waliokuwepo katika tukio hilo.

Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka huu katika kijiji cha Nyololo alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi hayo.

No comments:

Post a Comment