| Mch. Peter Msigwa akikabidhi vifaa vya michezo. |
Fifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2 vimetolewa na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.
Vifaa hivyo vilitolewa juzi ikiwa ni maandalizi ya Msigwa Cup linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi katika Manispaa ya Iringa.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na jezi na mipira na kuwataka wakazi wote wa Iringa kumuunga mkono na kukemea kila aina ya hujuma na vikwazo vinavyoweza kujitokeza.
Hata hivyo vifaa hivyo ni mwendelezo wa kutimiza ahadi zake alizoahidi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alipokuwa anomba kuchauliwa ili kuwawahikisha wananchi buneni.
“Moja ya ahadi nilizoziahidi wakati ninaomba ridhaa yenu ya uwakilishi bungeni ni kuboresha michezo, kwa hiyo ninatoa vifaa hivi kwa ajili ya maandalizi japo kuwa nilishaanza kutoa katika timu mbalimbali” alisema.
Miongoni mwa timu zilizopata vifaa hivyo ni pamoja na Don Bosco, Mawelewele, Jamaica. Hoho, Mlandege na Mgongo.
No comments:
Post a Comment