masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Friday, September 7, 2012

Siri za mauaji ya Mwangosi zaendelea kufichuka > Tendwa atakiwa kuwatumia wanasheria kuzijua taratibu

IGP Said Mwema
Wakati muuaji wa mwandishi wa habari katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten Daudi Mwangosi akielezwa kukamatwa, siri za mauaji hayo zinazidi kufichuka ndani ya jeshi la polisi Mkoa wa Iringa huku
kukamatwa kwa muuaji huyo zikiwa ni propaganda.

Mtaandao huu umeelezwa kuwa wengi waliokuwepo katika vikosi vya jeshi la polisi siku ya tukio ni mabaunsa wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao walikuwa katika mazoezi kutokana na mafunzo wanayopata katika makambi yao.

Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya jeshi lapolisi katika Mkoa huo kimeueleza mtandao huu leo kuwa Jeshi la polisi limechafuliwa na maofisa wao kutokana na kitendo cha kuwavalisha mavazi ya jeshi mabaunsa wa CCM kwa lengo la kufanya mazoezi kutokana na mafunzo wanayoendelea kupata katika makambi yao.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi ambacho kimeeleza kwa masherti ya kutoandikwa jina, kilisema kuwa jeshi la polisi limeingia lawamani kutokana na maofisa wake kukubali kuwapokea mabaunsa wa CCM na kuwapa silaha kwa nia ya kuwafanyisha mazoezi ndiyo maana wakati wote siku ya tukio walishindwa kuwasiliana na kamanda wa kikosi kutumia ishara za kijeshi na kuwa na hamu zaidi ya kupiga badala ya kufuata amri.

“Ni kweli hizi lawama hatuwezi kuzikwepa lakini sisi jeshi la polisi tulio wadogo hatuna makosa kwa sababu wengi wetu siku ya tukio walikuwa ni mabaunsa wa CCM waliotolewa kwenye makambi yao wanakopewa mafunzo na kuletwa kwa ajili ya mazoezi. Lawama zote hizi na kuchafuka kwetu kunasababishwa na maofisa wetu kukubali kuwavalisha mabaunsa wa CCM mavazi yetu” kilisema chanzo hicho.

Licha ya chanzo hicho kueleza hayo, kimeeleza kuwa RCO hana kosa kwa kuwa muda wote alionesha uungwana kuwa kikao kinachofanywa na CHADEMA ni cha ndani na kinafanyika kwa amani na kuwataka askari wasiingilie lakini kamanda wa mkoa ndiye aliyeamrisha askari kupiga raia.

“Kila wakati RCO wetu alikuwa akitutaka tusifanye chochote baada ya kuongea na viongozi wa Chadema kuonesha kuwa si mikutano ya hadhara bali ni vikao vya ndani ambavyo vilikuwa vikifanyika kwa amani lakini alipofika kamanda wa mkoa yaani RPC akaonesha kuwa na hasira na Chadema na kutuamuru kuwakamata viongozi wa chama hicho. Kwa kuwa mabaunsa waliokuwa wamevalishwa mavazi ya jeshi hawazijui ishara za jeshi badala ya kuwakamata viongozi wakaanza kutumia silaha na kuonesha dhamila ya kuua na kufanikisha walichotaka kukifanya” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kimeonesha kutokuwa na imani na kamanda wao Michael Kamuhanda kwa kile kilichoelezwa kuwa kamanda huyo anaonesha wazi kuwa ana chuki na Chadema na kutekeleza maagizo ya wakubwa kutoka juu.

“Tumetambua kuwa matukio hayo yote yanayotukia, ni maagizo ya wakubwa kutoka juu kwa kuwa RPC wetu anaonesha dhahili kuwa anatekeleza maagizo. Hakukuwa na sababu ya kutumia nguvu nyingi kiasi kile wakati watu wenyewe hawana hata vumbi tu mikononi mwao. Sisi wadogo tunaweza kutoa ushauri lakini lakini hatusikilizwi kwa kuwa mkubwa wetu akisema amesema. Ninyi waandishi na wananchi mtatuchukia bure sisi wadogo kwa kuwa daima tunatekeleza amri ya wakubwa wetu” kilisema chanzo hicho.

Kikizungumzia juu ya tetesi za kukamatwa kwa muuaji wa mwandishi huyo, chanzo chetu kimeeleza kuwa ni propaganda zilizoanza kutumika kwa ajili ya kulimaliza suala hilo kisiasa.

“Mwanangu, hizo ni propaganda ambazo zimeanza kutumika ili watu waamini kuwa kuna watu wamekamatwa lakini si kweli. Mimi binafsi pamoja na kuwa nipo ndani ya jeshi hilo sijui. Kuwa makini na taarifa hizo kwa kuwa zimeshaanza kutumika kisiasa ili kuwapiga mchanga wa macho watanzania” kilisema chanzo hicho.

Kumekuwa na simu nyingi taangu juzi kuwa askari watano wamekamatwa juu ya mauaji ya Mwanosi huku wengine wakieleza kuwa ni polisi wakitaka waandishi kufika katika kituo cha polisi kushuhudia askari hao
wakifikishwa kituoni jambo ambalo limekuwa likitia wasiwasi.

Jana asubuhi waandishi wengi katika mkoa huo walikuwa wakipokea simu kuwa askari 5 wanafikishwa mahakamani kutokana na mauaji ya mwandishi huyo lakini pamoja na waandishi hao kufika mahakamani kushuhudia, hakukuwa na askari yo yote aliyefikishwa mahakamani huko kutokana na tukio hilo.

Samabamba na chanzo hicho, wasomi wamemtaka msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa kutumia wanansheria kujua utaratibu badala ya kukurupuka na kuropoka asichokijua.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa George Tito ameuambia mtandao huu leo kuwa Tendwa hakupaswa kutoa kauli zisizo na hoja za msingi na badala yake anetumia wanasheria kuzijua taratibu.

“Ni dhahiri kuwa Tendwa hazijui sheria pamoja na kuwa nafasi aliyo nayo inahitaji sana kuzijua sheria. Licha ya kuwa hazijui sheria, alipaswa kuwatumia wanasheria kujua utaratibu kabla ya kukurupuka kutoka usingizini na kuropoka asichokijua. Ana kila sababu ya kuwaomba radhi watanzania ambao bado wanaendelea kuomboleza na matukio machafu yanayofanyikia na jeshi lapolisi nchini” alisema.

No comments:

Post a Comment