masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, September 22, 2012

Maandamano ya kumng'oa Kamuhanda yakwama Iringa > Polisi watoa visigizio > Mbunge achangia ujenzi wa shule

Baiskeli ya Mbungewa Iringa mjini iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili yake tayari kwa maandamano ya kushinikiza kamuhanda kung'ooka Iringa yaliyopangwa kufanyika jana.

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakizunguka kwenye magari kwa ajili ya kudhibiti maandamano.

Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa akitoa maelezo kwa waandamanaji juu ya barua aliyoipokea kutoka jeshi la polisi kutaka maandamano yasitishwe.

Mch. Peter Msigwa akiwasomea waandamanaji barua ya jeshi la polisi.

Waandamanaji wakisikiliza kwa umakini barua hiyo.

Mch. Msigwa akisukumwa kwenye baiskeli mara baada ya kuwatangazia wananchi kuahirishwa kwa maandamano.

Barua ya jeshi la polisi kutaka maandamano yasitishwe.

 
Inspekta wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema ameonja joto la kuzomewa na wananchi mkoani Iringa baada ya askari wa jeshi hilo kuzuia maandamano ya kumng’oa kamanda wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda.

Zomea zomea hiyo ilikuja baada ya muda mfupi kusitishwa kwa waandamanaji waliofika eneo hilo kwa ajili ya kuanza maandamano huku polisi wakiwa na magari zaidi ya manne kuhakikisha waandamanaji hawaingii barabarani.

Muda mfupi baada ya waandamanaji kuanza kutawanyika, yalitokea magari 3 ya makamanda wa polisi wa mikoa huku gari la katikati akiwemo IGP Mwema yaliyokuwa yakiingia katika jengo la ofisi kamanda Kamuhanda ndipo wananchi wakaanza zomeazomea.

Wakati wakiendelea na zomea zomea hiyo, magari ya kikosi cha kutuliza ghasia yakatokea na wananchi wakaanza kuwaimbia wimbo wakuwataka waende kuishi makambini kwao na kuacha mitaani walikopanga.

“Polisi tafuteni sehemu zenu za kuishi msirudi mitaani huku mlikopanga. Anayewatuma kutuua na kutupiga mabomu ndiye atakayewapa nyumba za kuishi. Mkirudi mitaani huku ama zetu ama zenu” waliimba wananchi.

Wakati wananchi wanaendelea kuimba, ofisa mmoja wa polisi alipita kwenye gari akasimama sehemu ndipo mtandao huu ulipoamua kumsogelea na kufanya mahojiano juu ya kuzuiliwa kwa maandamano hayo akasema wananchi wana haki ya msingi.

“Wanachodai wananchi ni haki yao ya msingi lakini tatizo ni sisi watoaji wa vibali hatuna upeo wa kuona mbali. Kuwataka polisi waliopanga mitaani waondoke nayo ni haki yao kwa sababu nao wana maamuzi kama tulivyo na maamuzi sisi katika kuwapa haki zao. Kilichokikubwa zaidi ni kwamba hatushauriki hata tungeshauriana sisi kwa sisi tunakuwa na vichwa vigumu wengine hawapendi kupokea ushauri. Nawaunga mkono wananchi kwa uamuzi wao ili na sisi tuone tabu ya kuwa na mahusiano mabaya na jamii” alisema osifa huyo.

Maandamano hayo yaliyotakiwa kufanyika jana kuanzia ofisi ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa yalikwamishwa na jeshi hilo kuwataka wananchi wasiandamane wakitoa sababu mbalimbali.

Awali Mch. Msigwa aliwataka wananchi kufanya maandamano ya amani kila wikendi kushinikiza Kamuhanda kuondoka Iringa kwa kuwa ameshindwa kuwatumikia wananchi na badala yake akafanya mauaji ya makusudi.

Gari alilokuwemo IGP Said Mwema aliyezomewa na wananchi kabla ya kuigia katika jengo la kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda.

Askari waliokuwa wakizunguka na magari eneo walipokusanyika waandamanaji baada ya kuahirisha maandamano na kutawanyika.

Gari la askari.


Magari ya maofisa wa polisi yaliyokubwa na dhahama ya kuzomewa na wananchi mjini Iringa jana


Katika hatua nyingine Msigwa ametoa vioo vyenye thamani ya shilingi 1,800,000/= katika shule ya sekondari ya Kihesa pamoja na Kompyuta kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo.

Akitoa vifaa hivyo amewataka wazazi kuwajibika kwa watoto wao ili kuwasaidia kupata elimu bora itakayowasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha yao ya kila siku.

“Wazazi na walezi wajibikeni kwa watoto wenu ili waweze kupata elimu itakayowasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha. Uwajibikaji wenu utawarahisishia kuwa wadadisi badala ya kuutumia muda wao katika kutafuta mahitaji ya muhimu” alisema Msigwa.

Msigwa akiwa mgeni rasmi katika Mahafali ya tatu ya shule hiyo aliwaasa wanafunzi hao kuwa wadadisi na kutumia elimu yao kwa kuhoji mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuonesha utofauti wa mtu aliyesoma na ambaye hajasoma.

“Elimu yenu mliyoipata itumieni katika kudadisi, kuhoji na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha; onesheni utofauti wa mtu aliyesoma na ambaye hajasoma kwa kutumia hoja za msingi. Hojini mambo yanayofanyika kwa kupitia misingi ya haki” alisema.

Aliwataka kuwa mabalozi wazuri katika kulinda mazingira kwa kuyaweka safi kwa kupitia rasilimali zilizopo.

“Mtaa hauwezi kuwa bora kama familia moja haijawa bora. Hali kadhali mazingira hayawezi kuwa bora kama mtu binafsi hajawa bora. Kuweni mabalozi wazuri wa kulinda mazingira kwa kuyaweka safi kwa kupitia rasilimali tulizo nazo kama vile misitu, ardhi na kuhakikisha kila sehemu inakuwa safi” alisema.

Hata hivyo alisema hawezi kugawa pesa kwa mtu mmoja mmoja bali atawajibika katika kazi za jumuiya  na vikundi mbalimbali.

“Kawaida yangu siwezi kumpa pesa mtu mmoja mmoja ila ninawajibika katika shughuli za pamoja katika jumuiya au vikundi. Kazi za kugawa pesa kwa mtu mmopja mmoja ni za mafisadi” alisema.

Wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari ya Kihesa wakiimba wimbo kuwaaga wenzao jana shueni hapo.

Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa (mgeni rasmi) akiwahutubia wanafunzi na wazazi waliohudhulia mahafali shuleni hapo jana.


Mch. Msigwa akiwakabidhi vyeti wahitimu wa kidato cha nne shuleni hapo.


Sambamba na hilo Msigwa alitoa mabati 50 na mifuko 4 ya sementi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1,000,000/= katika shule ya Msingi ya Ulonge Kata ya Ruaha ndani ya Manispaa ya Iringa kwa ajili ya kumaliza jingo la darasa linalojengwa shuleni hapo.

Akikabidhi shuleni hapo juzi alisema katika masuala ya maendeleo hakuna siasa wala ushabiki wa chama bali ni kuwajibika kwa ajili ya kusonga mbele.

“Katika masuala ya maendeleo ushabiki wa vyama na siasa usiingizwe bali uwepo uwajibikaji zaidi. Wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamepita sehemu mbalimbali kushinikiza wananchi wasipokee kitu chochote kutoka kwa viongozi wa upinzani. Wapuuzeni hao kwani ndio wanaorudisha maendeleo nyuma badala ya kupiga hatua mbele” alisema Msigwa.

Akizungumza na mtandao huu mara baada ya kupokea bati na sementi shuleni hapo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Maurus Mwilapwa alisema wananchi watoe ushirikiano kwa Mbunge huyo kwani ni mara ya kwanza kwa kiongozi ye yote kufanya hivyo shuleni hapo.

“Nashindwa hata kusema ndungu mwandishi kwa sababu hatujawahi kufanyiwa hivi katika shule yetu licha ya kuhusishwa katika chaguzi mbalimbali za viongozi, hatujawahi kumuona Mbunge au diwani katika shule yetu au kupata angalau chaki tu kutoka kwa kiongozi ye yote pamoja na kuwa tuna matatizo mengi. Naamini kabisa kuwa Mbunge ana dhamira ya dhati na nia ya kweli kwetu wananchi. Nawaomba wananchi wenzangu wa Iringa tumpe ushirikiano ili afanye kazi zake vizuri” alisema.

Mwenye magongo ni Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa mara baada ya kushuka kwenye gari katika shule ya msingi Ulonge.

Mch. Msigwa akiwahutubia wananchi wa Ulonge sambamba na kukabidhi mabati na sementi.

Baadhi ya wananchi wa Ulonge wakimsikiliza Mbunge Msigwa akikabidhi bati na sementi shule hapo.

Siment na mabati kabla ya kushushwa katika shule ya msingi Ulonge.

Wanchi wa Ulonge wakishusha mabati yaliyotolewa na Msigwa kwa ajili ya ujenzi wa dara katika shule yao.

Darasa linalojengwa katika shule ya msingi Ulonge kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa.


No comments:

Post a Comment