masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, September 11, 2012

Damu ya Mwangosi yalitesa Jeshi la Polisi Iringa > Wamepanga kulipuana > Mitutu yanukia ndani ya jeshi kumtaka Kamuhanda kuwajibishwa

Mwanahabari wa Mkoa wa Iringa wakiwa na bango kwenye maandamano









Damu ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten imeanza kulitesa  Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa kile kinachoelezwa kuwa askari wapo tayari kushika bunduki na kuanza mapigano ndani ya jeshi hilo endapo kamanda wao hatawajibishwa.

Taarifa zilizoufikia mtandao huu leo kutoka ndani ya jeshi hilo zimeeleza kuwa askari wamefikia hatua hiyo kushinikiza mwenzao aliyehusika na mauaji ya mwandishi huyo kutopelekwa mahakamani hadi hapo kamanda wao Michael Kamuhanda atakapowajibishwa kwa kuwa ndiye aliyehusika na tukio zima.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi ambacho hata hivyo hakikutaka jina lake kuandikwa kimeeleza kuwa hali ni mbaya ndani ya jeshi hilo kama haki haitatendeka dhidi ya watuhumiwa wa mauaji hayo.

“Tumefika pabaya ndani ya jeshi kwa sababu askari wadogo wamesema wamechoka kutumiwa na wakubwa kufanya vitendo vya kinyama ambavyo mwishowe vinawaletea mahusiano mabaya na jamii” kilisema chanzo hicho.

Kikizungumzia juu ya kutopelekwa mahakamani polisi aliyehusika na kifo cha mwanahabari huyo, chanzo hicho kimesema hawezi kupelekwa hadi hapo hali itakapokuwa shwari ndani ya jeshi hilo.

“Kikubwa ambacho kimesababisha hayo yote ni kifo cha mwanahabari Mwangosi kwa kuwa ndicho kilichoibua mambo mazito. Nikiwa miongoni mwa jeshi hilo sioni kama mtuhumiwa aende pekee yake mahakamani wakati alikuwa na wenzake na walitekeleza amri ya kamanda” kilisema.

Hata hivyo habari za ndani kutoka jeshi hilo zilizoufikia mtandao huu kwa siri zinasema kamuhanda alilazimika kutumia nguvu kutokana na pesa alizotoka kwa vigogo wa chama cha Mapinduzi wengine wakiwa mkoani hapa ambao majina yao yanahifadhiwa ili kuchafua Chadema na kuvuruga operesheni zilizokuwa zikiendelea.

“Naweza nikasema Kamuhanda ni jambazi kwa kutumia mashinikizo ya watu badala ya maadili ya kazi. Alipokea hela kama rushwa kutoka kwa vigogo wa CCM hapa mkoani waliomtaka ahakikishe kwa namna yo yote ile anachafua Chadema na kuvuruga mikutano yao. Pesa hizo alikula pekee yake akijua sisi hautujui na kwa bahati mbaya kijana wa watu ambaye hakujua chochote akaamriwa afyatue bomu. Kijana aliamriwa na kamanda bila kujua kinachoendelea na kama utakumbuka kila wakati RCO wetu alijitahidi sana kuzuia vijana wasitumie nguvu lakini RPC alipofika akataka kile alichokipanga na watu wake kitekelezwe” kilisema chanzo hicho.

IGP Said Mwema amelazimika kupiga kambi mkoani humo ili kufanya kikao na askari juu ya suala hilo baada ya hatua za awali zilizokuwa zikifanyika na jeshi hilo kwa mkoa wa Iringa kushindikana japo kuwa naye ameonja shubiri ya askari hao baada ya kushindwa kumwajibisha RPC mapema.

“Baada ya hali kuwa ngumu kutokuwa na maelewano baada ya mhusika wa mauaji kuchukuliwa hatua katika mahakama ya kijeshi, IGP Mwema amelazimika kupiga kambi katika mkoa huu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na vijana walioamua kufanya hukumu yao kwa RPC. Wamesema wako tayari kumnyanyulia bunduki RPC kutokana na hukumu iliyotolewa kiupendeleo wakiti yeye ni mhusika mkuu wa mauaji. Kwanza awajibike ndipo askari waliohusika wawajibishwe, naamini haki itatendeka vinginevyo mitutu itatugeukia sisi wenyewe kule ndani” kilisema chanzo hicho.

Katika hatua nyingine, wananchi wameonesha kuguswa na msiba wa mwandishi huyo pale walipoungana na waandishi wa mkoa wa Iringa na Tanzania leo kufanya maandamano ya amani wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti tofauti yaliyofikisha ujumbe kwa jeshi la polisi na serikali kwa ujumla.

Licha ya mabango hayo kuandikwa dukuduku walizonazo waandishi hao, bado waandishi wamebaki   na msimamo wao wa kutoshirikiana na jeshi la polisi huku wakitaka Kamuhanda ajitoe kwenye kiti kupisha uchunguzi huru kufanyika.

Hata hivyo waandishi wamelitaka jeshi la polisi kuchukua hatua kumsaidia mjane kwa kuwa hana kazi na watoto wanamtegemea huku likirudisha vifaa vya marehemu ambavyo alikuwa navyo wakati mauti akimkuta.

Vifaa hivyo ni pamoja na camera (video camera), laptop pamoja na simu yake ya mkononi.

No comments:

Post a Comment