| Stendi ya Miyomboni jinsi inavyozidiwa |
Stendi ya ya daladala Miyomboni katika Manispaa ya Iringa inazidiwa kwa kuwa na wingi wa magari na ongezeko la abiria.
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya madereva wa magari hayo wamelalamika kutozwa ushuru kila siku bila kuboreshwa stendi hiyo.
Abiria nao wameiomba serikali kuongeza eneo ili kukidhi haja ya mahitaji ya abiria hao.
Pamoja na ongezeko la magari na abiria, stendi hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma ya vyoo kwa abiria na wafanyabiashara wa maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment