UCHAGUZI wa serikali za Mitaa katika Mtaa wa Ngome Kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa umeanza kwa dosari licha ya kulazimika kuanza saa 6:04 mchana kutokana na kucheleweshwa vifaa vya kupigia kura.
Licha
ya vifaa vya kupigia kura kuchelewa, bado ilitokea dosari katika karatasi za
kupigia kura kwa kile kilochoonekana kwa baadhi ya majina ya waliogombea ujumbe
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoonekana kwenye karatasi za kupigia kura
na badala yake yakaingizwa majina ya watu wengine ambao hawakujaza fomu za
kugombea.
Sambamba
na hilo kwa upande wa wagombea kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), kuwa na kosa la waliogomea viti maalum kuingizwa jina la mwanaume
aliyegombea ujumbe huku mwanamke aliyegombea viti maalumu uingizwa kwenye
karatasi la wagombea wa ujumbe.
Sababu
hizi zimemlazimu wakala wa Chadema kutokubaliana na utaratibu huo na kutaka
utolewe ufafanuzi zaidi kabla ya kuanza zoezi la upigaji kura na kumlazimu
msimamizi wa uchaguzi wa kituo hicho kumpigia simu ofisa mtendaji wa Kata ili
aweze kutolea ufafanuazi jambo ambalo
pia lilimlazimu ofisa mtendaji kurudisha karatasi kwa mkurugenzi ili zifanyiwe
marekebisho.
Baada
ya maelezo ya ofisa mtendaji wa Kata ya Kihesa Wilbert Chahe kuwa kuna makosa katika
karatasi hizo, wananchi walipandisha hasira na kumzingira ofisa huyo jambo
lililowawalazimu vijana wa Chadema kumnusuru ili aweze kurudisha karatasi
zikarekebishwe.
“Ndugu
zangu wananchi na wapiga kura, nawaombeni kuwe na uvumilivu kuna tatizo
tumeligundua kwenye karatasi hizi lakini sisi ni watendaji tu, inabidi
nirudishe kwa Mkurugenzi ili yafanyike marekebisho. Kwa nawaombeni muwe
wavumilivu ili nishughulikie suala hili” amesema Chahe.
Baada
ya maelezo hayo wapiga kura walianza kupiga kelele huku wakimzingira, “acheni
uzuhi mmeanza mizengwe ili kukwamisha uchaguzi, huo ni mpango wa makusudi
mlioupanga ili uchaguzi usifanyike, tumechoka kuburutwa” zimesikika sauti hizo
huku wengine wakisema “umetumwa wewe, kawaambie waliokutuma kwamba tunajitambua”
zimesikika sauti hizo.
Wakati
wapiga kuwa wakisubiri karatasi kwa ajili ya kupiga kura, vijana walioaminika
kuwa ni viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM) walifika katika eneo la kituo cha
kupigia kura katika Mtaa huo na kuanza kuanza ushawishi kwa wapiga kura
kuipigia CCM jambo lililowatia hasira baadhi ya wapiga kura na kutoa taarifa
polisi.
Askari
polisi aliyekuwa akilinda usalama katika kituo hicho aliwatuma baadhi ya vijana
ili waaondoe viongozi hao mahala hapo kiustaarabu lakini viongozi hao walianza
kutumia nguvu kuwa hakuna wakuwatoa nakutangaza kupigana kufa na kupona.
Mmoja
aliyekuwa amevaa shati jeupe na suruali nyeusi anayeaminika kuwa ni katikabu wa
Umoj wa vijana Chama cha Mapinduzi (UV-CCM) Wilaya ambaye ni mkazi wa Mtaa wa
Kilimani alianza kutaka kurusha ngumi jambo lililomlazimu askari wa ulinzi
kuomba msaa kwa maaskari wenzake.
Wakati
mawasiliano ya askari na maaskari wengine yanaendelea, vijana wa Chadema ambao
wanaaminika kuwa ni walinzi (red-brigade) walituliza upepo ulioanza kuchafuka
na kuwataka watu kuwapuuza viongozi hao kwa kuwa nia yao si nzuri katika
uchaguzi.
Kila
mara red brigade walionekana kuwatuliza vijana waliokuwa na hasira kutaka
kutwangana na viongozi wa CCM ili kuwawezesha wapiga kura kuwa na amani.
Hadi
polisi wanafika katika eneo la tukio, walikuta vijana wa Chadema wameshayaweka
mazingira katika hali ya usalama na kuwaeleza polisi kuwa viongozi hao
walikimbia baada ya kuona gari la polisi linakuja na polisi wakawataka kutoa
taarifa haraka pale watakapoonekana katika mazingira hayo tena.
Wakati
huo huo wananchi wakisubiri karatasi za kupigia kura, baadhi ya wapiga kura waliokuwa wamekaa chini ya mti walisikika wakisema kuwa usiku wa kuamkia jumapili kuna baadhi ya watu
wanaoaminika kuwa ni wanachama wa CCM walikuwa wanapita wakigawa shiligi elfu
tano na maharage kilo moja moja kwa wapiga kura ili kuwashawishi wapiga kura
kuipigia kura za ndiyo.
Hata
hivyo wananchi wametaka kujua mwisho wa kupiga kura kutoka na kuchelewa kuanza
lakini msimamizi wa kituo amesema atawasiliaa na viongozi wa juu ili waone
kama wanaweza kuongeza muda wa kupiga kura katika kituo hicho.
No comments:
Post a Comment