masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, July 6, 2014

UJENZI WA MAKTABA ZA KIJAMII VIJIJINI WAANZA

Tuwafikie Tanzania wameanza kuhamasisha ujenzi wa maktaba ya jamii katika kijiji cha Lugalo, Kata ya Ilole, Wilaya Kilolo katika Mkoa wa Iringa.

Uhamasishaji wa ujenzi huo unakuja baada ya wanakiji kufyatua matofali kwa kushirikiana na wadau wengine kwa ajili ya kusaidia ukuaji wa elimu vijijini kwa jamii nzima.
Akizungumza na mtandao huu, mhamasishaji wa mradi huo Bovani Mwakyambiki amesema ili kufikia malengo ya mradi huo kwa ananchi asasi inategemea michango ya wananchi wenye kupenda mabadiliko ya kielimu na kwamba kila mmoja anayo nafasi ya kutoa ushiriki wake.
“Baada ya kuwaelimisha wanakijiji wa Lugalo na viongozi wa kijiji na kata, uongozi wa kijiji uliweza kutenga eneo, Uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na watendaji wa Tuwafikie wakahamasisha ushiriki wa wanakijiji katika ufyatuaji wa tofali.
“Nguvu kubwa ya kukamilisha zoezi hili ilikuwa ni ya wananchi wenyewe kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha lugalo, tanuri lilijengwa na tofali zikachomwa. Hivyo bado tunaendelea kusonga mbele na shughuli iliyopo mbele yetu ili tujenge kwa haraka maktaba hiyo na baadaye tuendelee mbele” amesema Mwakyambiki.
Ikiwa sehemu ya kujenga maktaba hiyo imekamilika, Mwakyambiki alisema wadau mbalimbali wa elimu na wale wanaopenda mabadiliko ya elimu wanayo nafasi ya kutoa michango yao kwa ajili ya kuendeleza gurudumu la ujenzi huo.
Amesema baada ya kuonana na kampuni ya interbeton iliyopo Mazombe na kuongea nao kuhusu uhitaji wa mchanga, mawe na kokoto, na baada ya kuwaeleza umuhimu wa maktaba ya kijiji kwa wanakijiji cha lugalo, kupitia mkurugenzi mkuu wa mradi wa ujenzi wa barabara Mr Hans Jorgen Kallehauge waliweza kupata mchanga na kokoto za kutosha
Licha ya kupata mchanga na kokoto za kutosha pamoja na tofali, asasi hiyo bado ina uhitaji wa fedha kwa ajili ya kununua saruji na Kukusanya mawe tayari kwa kuanza ujenzi.
Ameeleza kuwa harakati hizi zitahusisha wadau wote wa maendeleo ya elimu, kuanzia Marafiki wa elimu, Taasisi mbalimbali za kiserikari na zile zisizo za kiserikari, Makampuni na watu binafsi.
Amesema shughuli zote za Tuwafikie Tanzania ni shughuli zinazotegemea mwamko na ushirikiano wa wadau wote waliopo katika maeneo au mikoa husika.
“Hii itasaidia kufanikisha maono ya kuhakikisha Maktaba za Jamii zinajengwa na kupatikana maeneo ya vijijini ili kupunguza ujinga unaosababishwa na ukosefu wa Taarifa, ukosefu wa ujuzi na Elimu na Jamii kutokuwa na uwezo wa Kujitambua.
“Kuchangia mfuko wa Tuwafikie Tanzania ni Ishara ya kutuamini, na kitendo cha sisi kupokea mchango wako ni ishara ya Kujiamini na kuwa na hakika na kiu ya kutimiza malengo ya kuhamasisha maendeleo ya elimu vijijini kwa kushirikIana pamoja nawe” amesema.
Tuwafikie Tanzania ni Asasi iliyoanzishwa kuhamasisha Usomaji, Ujenzi na Matumizi ya Maktaba vijijini (Community Libraries).

No comments:

Post a Comment