masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, October 14, 2013

WATANZANIA WANA DENI KWA MWALIMU NYERERE: ASKOFU NGALALEKUMTWA

Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake.

Aliyevaa Mitra kichwa na kushikilia Pastoral Staff ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa, kushoto kwake ni Padre Victor Ngalembula Paroko wa Parokia ya Kihesa na kulia kwake ni Padre Paul Msombe Paroko wa Parokia ya Ipogolo wakati wa maadhimisho ya Misa ya kumkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilityofanyika leo katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Kihesa Jimbo la Iringa.

Shirikisho la Kwaya za Parokia ya Kihesa, Kwaya ya Mtakatifu Cecilia (Kwaya Kuu), Kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu na Kwa ya Mtakatifu Paul wakiimba kanisani wakati wa maadhimisho ya Misa ya kumkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Waziri Stiphen Wassira akiwa kanisani hii leo.

Baadhi ya Mapadre wakiwa kanisani wakati wa maadhimisho ya Misa ya Kumkumbuka Baba wa Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma pamoja na viongozi wengine wakiwa kanisani wakati wa maadhimisho ya Misa ya kumkumbuka Baba wa Taifu Mwalimu Nyerere.

Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Madiwani na viongozi wengine akiwemo mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) (mwenye mavazi ya kijani) wakiwa kanisani wakati wa Misa ya kumkumbuka Baba wa Taifa hii leo.

Kushoto ni Spika wa Bunge Mama Anne Makinda, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma, kushoto kwa Mkuu wa Mkuu wa Mkoa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Philip Mangula akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jescar Msambatavangu wakiwa kanisani.

Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akipokea matoleo kanisani.

Shemasi Paul akisoma somo la Injili kanisani.

Waziri wa Serikiali za Mitaa (TAMISEMI) William Lukuvi na nyuma yake Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Peter Msigwa (CHADEMA) wakifuatilia Misa Takatifu kanisani.
Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake.


RAIS wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema Watanzania tuna deni kubwa ambalo ni jukumu la kila mmoja kulipa.

Ameyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu iliyokuwa ni kwa ajili ya kumkumbuka Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika kitaifa mkoani Iringa katika Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Parokia ya Kihesa (Kanisa Kuu la kiaskofu).

Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa Jimbo la Iringa na msimamizi wa Jimbo Kuu la Songea amesema deni linalopaswa kulipwa ni kufuata maadili na matendo ya haki.

“Tuna deni kubwa kwa Hayati Baba yetu wa Taifa na deni hilo lazima lilipwe. Deni hilo ni kuishi kwa pamoja kwa umoja na kuheshimiana pia” amesema.

Amesema watanzania walipewa zawadi kubwa ambayo kwayo amani ya nchi ilijengeka na heshima ya nchi ilipatikana ambapo kila mmoja anawajibu wa kulinda tunu hizo.

“Maisha yake yalikuwa zawadi kwetu; si kwa watanzania pekee bali kwa waafrika na dunia nzima” amesema.

Amesema Mwalimu alijitahidi kutunza roho ya mcha Mungu huku kazi zake akizifanya kwa hofu ya Mungu.

Pia amesema Mwalimu alijitahidi kukusanya watanzania katika kaki na kuwajengea moyo wa kumtegemea Mungu jambo lililosaidia kulinda heshima ya nchi.

“Tusivunje matumaini kwa Mungu. Tuzitoe nafsi zetu katika kujali Mungu na wenzetu. Tuishi kwa uchaji ili Mungu atushushishie Baraka zake. Tukiishi kwa uchaji, hata wale hata wale tunaoishi nao watatunza kumbukumbu tamu, nzuri na nono katika mioyo yao” amesema.

Hata hivyo akofu Ngalalekumtwa amewataka watanzania kuishi kwa kuheshimia katika imani ili kuendeleza utamaduni wa kuishi kwa pamoja bila kutofautiana kwa kwa kigezo cha imani na kwamba binadamu anahitaji huruma, ya Mungu, faraja na utakaso kwa yale machafu anayoyafanya au kuwafanyia binadamu wenzake.

Aidha amewataka viongozi wa ngazi zote kuwa na roho ya huruma, upendo na kuwatendea raia wake haki inayostahili.

“Kupitia Misa hii tuliombee Taifa letu, viongozi wetu ili wawe na roho ya huruma, upendo, upole na haki. Haya yakiwepo tukawa na viongozi wa namna hiyo, nchi itabaki kuwa ya amani.

“Tunapenda nchi iwe ya amani. Zifike nyakati za amani, za kutulia na nyakati za kutazamana kwa raha. Uhuru wa kuabudu uheshimiwe. Anayeviruga uhuru huu si mwenzetu na huyi ndiye anayeingiza machafuko kwa watu wanaopenda amani” amesema

No comments:

Post a Comment