 |
| Hawa ni baadhi ya ndugu waombolezaji waliokuwa kando ya kaburi. |
 |
| Jeneza likuwa limeshafikishwa kando ya kaburi tayari kwa mazishi. |
 |
| Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo la Mbeya mwenye vazi jeupe na askofu Tarcisius Ngalalekumtwa mwenyevazi jeusi wakiwa kando ya kaburi, |
 |
| Jeneza likiwa limefungwa kamba na kushushwa kaburini. |
 |
| Jeneza likishushwa kwenye kaburi. |
 |
| Baada ya jeneza kushushwa kawenye kaburi. |
 |
| Watu mbalimbali wakiweka udongo kwenye kaburi. |
 |
| Mapadre Victor Ngalembula akimnong'oneza jambo mwenzake padre Mkalawa. |
 |
| Hii ni karuri baada ya kuzika. |
 |
| Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akiweka shada juu ya kaburi. |
 |
| Mhashamu askofu Evaristo Chengula wa jimbo la Mbeya akiweka shada juu ya Kaburi. |
 |
| Dada wa marehemu akilia baada ya kuweka shada juu ya kaburi. |
 |
| Watoto wa shirika la Kipapa wakiweka mashada juu ya kaburi baada ya mazishi. |
 |
| Masista na wawakilishi wa Parokia ya Nyakipambo wakiwasha mishuma katika kaburi. |
 |
| Mwenyekiti wa umoja wa mapadre jimbo la Iringa (UMWAI) Padre Cephas Mgimwa akitoa pola na shukurani kwa watu mabalimbali. |
RAIS wa Baraza la Maaskofu
Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema jimbo la iringa limepata pigo
kubwa kwa kifo cha Padre Liberatus Mwenda.
Akizungumza wakati wa mahubiri
katika Misa ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Moyo Mtakatifu Parokia ya
Tosamaganga Jimbo la Iringa, askofu Nagalalekumtwa alisema pengo alilolicha
padre Mwenda ni kubwa na kwamba linaleta simanzi.
“Tuseme nini? Hatuna ugomvi na
Mungu lakini yeye ndiye aliyeamua kama alivyomuumba. Tumsindikize kwa sala na
maombi ili akapumzike kwa amani” amesema.
Amewaasa wakristo kuishi kwa
upendo, haki na uadilifu ili kutendeana mema hapa duniana na kuacha uonezi wa
makusudi kwa wengine.
“Kwa kuishi katika upendo, haki,
na uadilifu katika injili, tuna uhakika wa kuufikia muunganiko na Mungu. Maombi
haya ya leo iwe nguvu ya maisha yetu pamoja na kusindikiza safari ya mwenzetu
kwenda kupumzika” amesema.
Hata hivyo amewataka wakristo kukubali
mipango ya Mungu na kumshukuru kwa zawadi aliyotoa na kumuomba Mungu ampokee padre
Mwenda katika umoja wake wa malaika.
Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia
ni askofu wa jimbo la Iringa na mlezi wa Jimbo Kuu la Songea amewataka wakristo
kuomboleza kwa imani na amani ili kuendeleza utulivu katika nchi.
Amesema padre Mwenda katika uhai
wake alishiriki kazi za kichungaji na kimaendeleo katika ustawi wa Kanisa na
wake na kwamba alikuwa mhudumu wa kwanza katika nyumba yajimbo Nazareth iliyopo
katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Padre Liberatus wakati wa uhai
wake aliwahi kufanya kazi katika jimbo la Agrigento – Cicilia Italia na aliteuliwa
kuwa mlezi wa vyama vyama vya kipapa vya kimisionari.
Alizaliwa Septemba 25, 1955
katika Parokia ya Wasa.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo mhashamu askofu Evaristo Chengula wa jimbo la Mbeya, sekretarieti ya baraza la maaskofu Tanzania, viongozi mbalimbali wa madhehebu na serikali kutoka sehemu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment