masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, July 21, 2013

MBUNGE ASEMA MPANGO WA KUWAPIGANIA MACHINGA HAUJABADILIKA





Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa (Chadema) akihutubia wakazi wa Kihesa katika Manispaa ya Iringa.






MBUNGE wa Iringa mjini Peter Msigwa (CHADEMA) ameendelea kusisitiza kuwa pamoja na kuwa suala la wafanyabiashara ndogo (machinga) wa mashinetatu liko mahakamani, ataendelea kupigania ili kuhakikisha hawaondolewi nje ya mji.

Msigwa amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara wa kiserikali uliofanyika katika uwanja wa Kihesa katika Manispaa ya Iringa na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu na ili wakati akiendelea kufanya taratibu za kisheria kuwapigania haki zao.

Amesema machinga ni watu wanaopaswa hithaminiwa kwa kuwa wanalipa kodi zao kama kawadi sawa tu na watu wengine na kwamba inapofika mahala wananyanyaswa familia zao zinadorora.

“Pamoja na kuwa suala la Machinga pale mashinetatu lipo mahakamani, mpango wangu kuhakikisha hawatolewi nje ya mji upo palepale” alisema Msigwa.

Amesema watu wengi wanafikiri kuwa cheo kinabadilisha akili ya mtu jambo ambalo wengine wamegeuka kuwa miungu wangu kwa kutaka waheshimiwe na kupigiwa saluti hata wanapofanya viba.

Amesema licha ya kuwa watu huchagua viongozi wao kwa kusudi la kuwawakilisha, wapo ambao baada ya kupata vyeo wamekuwa tofauti na matarajio ya wananchi na kugeuka kuwa kikwako kikubwa kwa maisha ya wananchi.

“Kuna watu tumewapatia vyeo lakini ni wapumbavu. Cheo hakibadilishi akili. Kama huna akili ukipata cheo utabaki kuwa mpumbavu tu” amesema.

Pia amesema ikiwa mtu anajua kusoma na asijishughulishe na kujisomea atakuwa hana utofauti na mtu ambaye hakusoma kabisa na kwamba wajibu wa viongozi ni kutatua shida za wananchi wake lakini wengi wamekuwa wababaishaji tu.

Naye Dady Igogo kutoka jimbo la Rorya amesema kiongozi anayechaguliwa na watu kuwa muwakilishi na kugeuka kuwa bubu ni hatari katika ustawi wa jamii na maendeleo kwa ujumla.

“Ukiona una muwakilishi ambaye hawezi kuzungumzia kero za watu wake ni hatari. Kiongozi wa namna hiyo hafai kuendelea kuwa muwakilishi na pia anakuwa ametudharau tuliyempa dhamana hiyo.


“Msigwa ni nyuki ambaye hakumbatiwi na watu wahuni. Wote wanaombeza Msigwa ni wahuni ambao wanataka kufanya mambo yao kihuni. Tusikubali kuendelea kuwa na wahuni. Tuwakatae watu wa mtindo huo” alisema Igogo.

No comments:

Post a Comment