masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Friday, May 31, 2013

VIONGOZI WA CCM WAONJA JOTO LA JIWE, WALIVAMIA UWANJA WA MKUTANO KUTAKA KUFANYA MKUTANO BILA KIBALI

Nape Nnauye


VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameonja joto la jiwe baada ya kufukuzwa kwa nyengo na shoka katika kata ya Ng’ang’ange walipofika kuvamia kiwanja kwa ajili ya mkutano bila kibali cha mwenye kiwanja.


Hayo yalitokea jana katika kijiji cha Mdeke ambapo walifika jioni kwa ajili ya kufanya mkutano bila kuomba kibali cha mwenye kiwanja na kujikuta katika wakati mgumu baada ya familia inayomiliki kiwanja hicho kutokea wakiwa na silaha na kuwavurumusha.

Dhahama hiyo iliwakuta viongozi wa CCM akiwemo mwenyekiti wa chama hicho wa Iringa mjini Said Kiponza na mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kilolo Sifuni Makongwa.

Akiongea na mtandao huu mmoja wa familia hiyo ambaye ameomba jina lake lisiandikwe gazetini alisema imefika wakati sasa kukataa kudharaulika na watu wanaotaka kutumia madaraka yao kwa manufaa yao binafsi.

“Ni kweli tumefanya hivyo kwa sababu tuliona ni dharau kubwa. Eti mtu anakuja nyumbani kwako bila kupiga hodi na kuanza kufanya atakacho kana kwamba hakuna mwenye nacho. Hii inaonesha jinsi walivyo na mabavu kutaka kila kitu kuwa ni chao eti kwa kuwa wapo madarakani.

“Kwa nafasi hii napenda kuwaambia kuwa muda wa kunyanyasika umekwisha. Sasa tuheshimiane, hakuna mtu ambaye yupo usingizini sasa hivi kama walifikiri bado tupo usingizini wamechemka. Na kibaya zaidi kwa nini waje usiku kama siyo unyang’anyi huo” kimesema chanzo chetu.

Sifuni Makongwa alipotafutwa kwa njia ya simu ili kutolea ufafanuzi wa kile kilichodaiwa na familia hiyo amesema hakuwepo katika tukio hilo na kwamba hajui ni nani yupo kule ambaye anaweza kutoa maelezo.

“Mimi sikuwepo katika tukio hilo. Nipo mjini lakini sijajua ni nani yupo kwenye kampeni huko Ng’ang’ange ambaye anaweza kukupatia majibu!” amesema.

Hata hivyo Kiponza alipoulizwa kwa njia ya simu alikiri kuwepo na tukio hilo na kwamba hayo ni mapito tu.

“Si unajua mambo ya hapa na pale! Ni Bibi kizee mmoja pamoja na wanawe walituletea usumbufu kidogo lakini tumemalizana nao. Ni kweli hakukuwa na taarifa ya kufanya mkutano hapo lakini basi yametokea tutarekebisha yasitokee tena” amesema Kiponza.

Alipotakiwa kufafanua zaidi ni kwa nini kufanya mikutano kwa kuvamia, Kiponza hakuwa na jibu.

Katika hatua nyingine mikakati ya kutaka kumrubuni mgombea udiwani katika kata hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Nafred Lucas Chahe imegundulika.

Taarifa zilizopatika ndani ya CCM zimeeleza kuwa waameandaliwa watu maalumu kwa ajili ya kuhakikisha mgombea huyo anarubuniwa kwa gharama yoyote na kwa njia yoyote ili mradi wakati wa uchaguzi asipite.

Kwa mujibu wa chanzo chetu taayari mipango ya kuanza kumtafuta mgombea huyo kwa ajili ya kuingia mkenge imeanza na sasa ameanza kupigiwa simu ili kukutana na watu hao.

Alipotafutwa kwa ajili ya kuthibitisha, mgombea huyo alikiri kupigiwa simu mara kadhaa na watu tofauti tofauti kutaka wakutane naye Katika kijiji cha Kidabaga na wakati mwingie wakitaka kukutana naye mjini.

“Ni kweli napigiwa simu mara nyingi wakitaka nikutane nao eti kwa madai kuwa wanataka kuniongezea uwezo wa kupiga kampeni lakini nakataa kila wakati na sehemu wanazotaka nikutane nao si nzuri kwangu” amesema Chahe.

Namba zinazotumika kumpigia mgombea huyo ili kukutana yane zimetajwa (tunazo zinahifadhiwa).

Katika utafiti uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa namba zilizotajwa kutumika wamiliki wake wote ni kada wa CCM

No comments:

Post a Comment