masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, December 6, 2012

Ajali iliyoteketeza familia hii


Watu sita wanaosadikika kuwa wa familia moja wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Tanangozi, kata ya Mseke Mkoani Iringa, walipokuwa wakisafiri kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kyela Mkoani Mbeya.
Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa Gwanchele Faustine amethibitisha kupokea maiti sita ikiwemo ya mtoto mmoja Erick Mwaikeleke anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi 6 hadi mwaka 1, Ezekiel Mwakeleke, Grace

Mwakeleke na Happy Mwandike msaidizi wa kazi katika familia ya Mwaikeleke, aliyesadikika kupandia gari hilo maeneo ya Ilula Wilayani Kilolo Mkoani Mringa.
Gwanchele alisema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gari ndogo kugonga Semi-Trailer wakati Dereva wa gari hiyo alipotaka kuzipita roli zilizokuwa mbele yake katika foleni ili aweze kuwa karibu na geti na pengine kuwa wa kwanza kutoka pindi zitakaporuhusiwa ndipo aliposhindwa kutokana na gari zilizokuwa zimesimama mbele yake katika foleni kuruhusiwa, hali ambayo ilimfanya dereva wa gari ndogo hiyo kutafuta upenyo ili kupisha gari hizo, ndipo alipoliingia Roli hilo kwa haraka na kusababisha ajali hiyo.
Aliongeza kuwa baada ya ajali hiyo kutokea watu wanne walifariki hapo hapo, mwingine alifia mapokekezi katika hospitali hiyo ya Rufaa, na wa mwisho alifia wodini, ambapo maiti tano ziliweza kutambulika kwa majina na mbili hazikuweza kutambulika kwa haraka.

Mmoja wa shuhuda wa ajali hiyo ambaye hakutaka jina lake lifahamike alisema kuwa, ajali hiyo ilitokea maeneo ya Tanangozi majira ya saa sita na nusu mchana ambapo gari ndogo aina ya RAV 4 yenye nambari za usajiri T 566 BNQ lilikuwa likiendeshwa na Ezekiel Mwaikeleke mkazi wa Sinza jijini Dar es salaam, liligonga gari aina ya Semi lenye namba za usajiri T 840 DFT Scania na kusababisha vifo vya watu sita waliokuwa katika gari ndogo.




No comments:

Post a Comment