| Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Iringa Rosalia Mwenda akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo. |
| Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa katikati, Meneja Msaidizi Swalehe Byarugaba kulia na Meneja Msaidizi - Madeni na Ulipaji kodi kwa ridhaa Salehe Kiluwa kushoto. |
| Mr. Hilly mfanyakazi wa TRA kushoto na Mr. Ipyana Mwakalinga mhasibu wa TRA Mkoa wa Iringa kulia. |
| Godfrey Mushi mwandishi wa Nipashe akimsikiliza meneja wa TRA. |
| Laurian Mkumbata mwandishi wa ITV na Radio One akiandika habari katika ofisi ya meneja wa TRA. |
| Zulfa Shomari mwandishi wa Mwananchi akiandika habari katika ofisi ya meneja wa TRA. |
Mamlaka ya mapato Mkoa wa Iringa
imekusanya zaidi ya shilingi 24 bilioni zaidi ya kiwango walichopangiwa na
serikali kukikusanya kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012.
Taarifa hiyo imetolewa leo na
meneja wa mamlaka ya mapato katika Mkoa huo Rosalia Mwenda alipokuwa akiongea
na vyombo vya habari ofisini kwake.
Kiasi hicho ni zaidi ya kile
kilichopangwa na serikali kukusanywa kwa muda huo ambapo jumla ya shilingi 23
bilioni zilitakiwa kukusanywa.
Kodi hizo zilizopangwa kukusanywa
ni pamoja na ushuru wa forodha pamoja na kodi za ndani.
Taarifa hiyo imetolewa wakati
mamlaka ya mapato inaadhimisha siku ya mlipa kodi ambayo kilele chake
kinatarajia kufanyika Novemba 7, mwaka huu ambayo katika Mkoa wa Iringa
itafanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria.
Wakati wa maadhimisho ya siku ya
mlipa kodi, mamlaka ya mapato katika Mkoa huo, jumla ya shilingi 877,000,
zimekusanywa kwa ajili ya kutoa msaada wa kibinadamu katika kituo cha kulelea
watoto yatima cha kiislamu cha Dhinurayn kilichopo Ilala mkoa ni humo.
Wakati akitoa taarifa hiyo,
Mwenda amewataka wananchi kutoa maoni juu ya huduma zinazotolewa na mamlaka
hiyo ili palipo na mapungufu yafanyike marekebisho kwa ajili ya kusimamia haki
pamoja na kutoa mafunzo kwa wanafunzi mbalimbali juu ya masuala ya kodi.
“Katika maadhimisho hayo,
tutatumia fursa hii kupokea maoni ya wateja na wadau mbalimbali juu ya huduma
zetu ili pale ambapo panakuwa na mapungufu tuweze kurekebisha ili kutoa huduma
kwa haki na pia tutatoa semina kwa wanafunzi kuhusu masuala ya kodi ili wawe
wasambazaji wetu wa taarifa na watoaji wa elimu kwa watu mbalimbali” amesema
Mwenda.
Ikiwa maadhimisho ya siku ya
mlipa kodi huambatana na kauli mbiu, mwaka huu maadhimisho hayo yanabebwa na
kaulimbiu inayosema “Ulipaji Kodi wa Hiari kwa Taifa Lenye Mafanikio”.
Katika kufanikisha ukusanyaji wa
mapato hayo kwa mwaka 2011/2012 njia mbalimbali zilitumika ikiwemo ya kutoa
semina kwa walipakodi, kutoa huduma bora kwa wateja, kutoa mafunzo ya kodi kwa
wanafunzi pamoja na kuhamasisha walipakodi kwa njia ya redio na matangazo.
Amesema kuna sababu ambazo
zinaweza kukwamisha ukusanyaji wa kodi kwa wateja ikiwemo ja kudorora kwa hali
ya uchumi duniani ambako huchangia kwa kiawango kikubwa kupotea kwa pato la
serikali pamoja na kushuka kwa makusanyo ya kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).
Lengo la maadhimisho ya siku ya
mlipakodi ni kutambua ushiriki wa walipakodo katika kuhakikisha kuwa na ulipaji
kodi wa hiari kwa Taifa.
Ikiwa Novemba 7 yatakuwa ni
maadhimisho ya sita, Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa watawatunuku vyeti jumla
ya walipakodi 24 ambao wapo mstari wa mbele katika kuweka kumbukumbu za za
biashara kwa usahili, kulipa kodi zinazolingana na biashara zao, kujituma
kulipa kodi kwa wakati kisheria na wale wanaolipa kodi zao kwa hiari.
Hata hivyo Mwenda amesema
wanaendelea kufuatilia madeni kutoka kwa walipakodi ambapo kiashi cha shilingi
1 bilioni hazijalipwa kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali.
“Pamoja na kuvuka malengo, wapo
walipakodi mbalimbali ambao wanadaiwa bado hawajalipa kodi zao. Madeni hayo ni
ya muda mfupi nay ale ya muda mrefu ambapo hivi sasa kiasi ambacho walipakodi
wetu wanaodaiwa ni shilingi bilioni 1. Tutahakikisha kuwa wanalipa kwa kutumia
njia mbalimbali pamoja na wadau wengine wanaokusanya kodi hizo” amesema.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
ilianza kusherehekea siku ya mlipakodi mwaka 2006 ilipotimiza miaka 10 tangu
kuundwa mwaka 1997.
No comments:
Post a Comment