masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, September 3, 2012

Tamko la Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa lililotolewa leo baada ya kuuawa mwenyekiti wa Chama hicho Daud Mwangosi

KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC) na waandishi wa habari wote mkoani Iringa na nchini kwa ujumla wamepokea kwa mshutuko na masikitiko makubwa kifo cha Mwenyekiti wa IPC, Daudi Mwangosi.
 
Mwangosi ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa Channel Ten, alifariki jana majira ya saa 10 jioni baada ya kupigwa bomu katika vurugu za wafuasi wa Chadema waliokuwa wakitawanywa na jeshi la Polisi.
 
Utata wa nani anahusika na tukio hilo umeendelea kugubika huku jeshi la Polisi likitoa tamko linalodhihirisha dhahiri kwamba wanataka kujiondoa katika kosa hilo kabla uchunguzi haujafanyika.
 
Katika taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na Polisi hii leo imedai kwamba bomu linalodaiwa kumuuawa mwandishi huyo lilitoka katika kundi la wafuasi wa Chadema, wakati Mwangosi akitafuta msaada wa kujinusuru kwa askari waliokuwepo katika eneo hilo.
 
Lakini wakati jeshi hilo likitoa taarifa hiyo inayokinzana yenyewe, limeshindwa kueleza ni kwasababu gani bomu lililorushwa kutoka katika kundi la wafuasi hao likamdhuru na kumuua mwandishi huyo pekee yake wakati alikuwa ameshikiliwa na mmoja wa askari wa jeshi hilo baada ya kupigwa virungu alipotaka kujua sababu ya kukamtwa kwa mwandishi mwingine Godfrey Mushi aliyekuwa akipiga picha tukio hilo.
 
Uchunguzi wa awali wa IPC unapingana kwa asilimia zote na taarifa ya jeshi hilo kwa kuzingatia taarifa zilizotolewa na baadhi ya waandishi waliokuwepo katika tukio hilo na zile zilizoandikwa na kurushwa na vyombo mbalimbali vya habari toka jana.
 
Taarifa kutoka katika vyanzo vyetu zinaonesha kwamba Mwangosi alipigwa kwa virungu kabla ya kulipuliwa na bomu hilo ambalo kwa vyovyote vile muhusika wake mkuu anaweza kuwa jeshi hilo.
 
Ili taarifa hiyo potofu isiendelee kuugubika umma, IPC imeamua kutoa tamko linalolenga kuviarifu vyombo huru viiingilie kati katika uchunguzi huo.
 
Na kwa kuzingatia mazingira hayo, IPC kwa kushirikiana na waandishi wote wanaofanya kazi mkoani Iringa, kuanzia leo wanatangaza rasmi kusitisha ushirikiano wa kikazi baina yao na jeshi hilo mpaka pale taarifa au majibu sahihi kutoka kwa vyombo huru vitakavyolifanyia kazi suala hilo yatakapotolewa.
 
Kazi hizo ni pamoja na kuwataarifu waandishi wa habari kusitisha mara moja kwenda katika Ofisi ya RPC kwa ajili ya kupata taarifa za matukio mbalimbali ya uhalifu yanayotokea kila siku.
 
Aidha IPC inawataka wanachama au viongozi wake waliokuwa wajumbe wa kamati zozote zile zinazolihusu jeshi hilo ikiwemo ile ya maandalizi ya wiki ya usalama barabarani kujitoa kwenye kamati hizo.
 
IPC inawaomba waandishi wa habari kushikamana katika kipindi hiki kigumu kwa kuzingatia kwamba  yaliyomkuta ndugu yetu Mwangosi yanaelekea kumkuta mwandishi yoyote Yule nchini.
 
Tukio hilo linadhihirisha jinsi uhuru wa  habari na vyombo vya habari unavyozidi kukandamizwa hasa katika kipindi hiki ambacho watanzania kwa ujumla wao wanatakiwa kushiriki kikamilifu kuandika Katiba Mpya wanaoitaka.
 
Tukio hilo haliwezi kuvumiliwa na kwa msimamo huu, IPC inaomba waandishi wote wawe na wimbo mmoja utakaowezesha muhusika wa mauaji hayo akamatwe na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
Pamoja na kukamwata kwa muhusika, IPC inataka kuona jeshi la Polisi ambalo kimsingi halipo juu ya sheria linatimiza wajibu wake kwa kuzingatia sheria kama ilivyo kwa taasisi zingine.

Aidha kwa  sasa  wanahabari  mkoa  wa Iringa  tunatangaza  rasmi  kusitisha mahusiano  yetu na jeshi la  polisi  kwa  kuandika habari  za  polisi .

Pia tunatambua  kuwa wakati Mwangosi  akikamatwa alikuwa katika  kutimiza  wajibu wake kama  mwanahabari  hivyo hata kama alikosa kwa  kufika hapo hukumu  yake haikuwa  kuuwawa  .

Hivyo kutokana na  tukio  hilo  kubwa ambalo halikuwa na  chembe  ya  siasa  kwa  mwanahabari  huyo kwa  kuwa hakuwa ni kiongozi  wa chama  cha Siasa IPC na Chanel Ten kama mwajiri  wake na familia tunachukua dhamana ya  kusimamia mazishi  hayo  bila huku  tukiviomba  vyama  vya siasa kutovuruga taswira ya Tasnia  hii ambayo kamwe haifungamani ya chama  chochote  cha  Siasa .
 Na tunalitaka jeshi la Polisi litoe ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi na za kweli kwa makundi huru yanayoendelea kulichunguza suala hilo.

Kifo cha Mwangosi  kimetufanya  wanahabari kote nchini  kujipanga  upya katika  kutathimini upya mahusiano  yetu na jeshi la  polisi .
Mungu ailaze mahali pema roho ya Marehemu  Daud Mwangosi. Amin

Francis Godwin
katibu  msaidizi IPC

No comments:

Post a Comment