masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, September 22, 2012

Mch. Msigwa atoa vifaa vya michezo kwa wachezaji wa mpira wa miguu Iringa

Baadhi ya wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Ulonge wakiwa wamevaa jezi mara baada ya kupokea kutoka kwa Mbunge Mch. Peter Msigwa.


Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa ametoa vifaa vya michezo katika timu mbalimbali za mpira wa miguu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 6 milioni.

Msigwa alitoa jezi na mipira juzi katika timu hizo ikiwa ni maandalizi ya shindano la Msigwa Cup linalotarajiwa kuanza ndani ya Manispaa wiki chache zijazo.

Baadhi ya timu ambazo zimepewa vifaa hivyo ni pamoja na timu mbalimbali ikiwemo timu ya mpira ya shule ya sekondari ya Kihesa, timu za vijana wa Kihesa, Mivinjeni pamoja na timu ya vijana ya Ulonge.

Akikabidhi vifaa hivyo, Msigwa alisema viongozi wa timu za mpira wanatakiwa kuwa na umoja na si marumbano.

“Tatizo la timu zetu hizi ni uongozi. Hatuwezi kusonga mbele kama kila siku katika timu zetu ni malumbano tu. Tujaribu hata kubadilisha mfumo wa uongozi wetu ili tusonge mbele” alisema.

Alisema sababu nyingine ni viongozi kuendekeza ubinafsi na kutafuta maslahi badala ya kuendeleza soka.

“Tuache kuweka maslahi mbele na ubinafsi badala ya kuendeleza soka. Mifumo tuliyonayo ibadilishwe ili tupige hatu mbele” alisema.

No comments:

Post a Comment