masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, June 7, 2012

Kongamano la Ekaristi Takatifu Kitaifa laanza Iringa







Picha ya pamoja Maaskofu, Mapadre na watawa baada ya kutoka kanisani

Wakristo wametakiwa kumkabidhi Mungu kwa Roho na kweli viashilia vyote
vya uvunjifu wa amani ili viweze kutokomezwa kwa njia ya upendo na
mshikamano.

Haya yamesemwa leo na Mhashamu Baba Askofu Yuda Thadeus RuwaIchi
alipokuwa akihubiri katika Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Parokia ya
Kihesa Jimbo Katoliki la Iringa katika Misa ya ufunguzi wa Kongamano
la Ekaristi Yakatifu.

Akizunumzia tukio lililotukia hivi karibuni huko Zanzibar alisema kuwa
Mungu hawezi kupendezwa na hali hiyo kwa kuwa ni kinyume na utaratibu
na ukiukwaji mkubwa wa sheria na kuwaomba watu wote kushirikiana
kukemea.

Alisema viashilia vinayotokea sehemu mbalimbali kwa nyakati tofauti
vinasababishwa na watu kukosa upendo, kutowajali wengine na ubinafsi
wa wachache hivyo havina budi kukomeshwa.

“Kama sisi wewenyewe tunapendana, uvunjifu wa amani na viashilia kama
hivyo haviwezi kujitokeza. Ubinafsi wa wachache ndio unaweza
ukatupeleka katika bagombano na huhitilafiana, tushirikiane kuvikemea
vitendo hivyo” alisema Mhashamu RuwaIchi.

Aliwataka wakristo wakati wote wa maadhimisho hayo walikabidhi Taifa
mikononi mwa Mungu, dunia na kumkabidhi matatizo yote ili dhambi
ziweze kusamehewa ili amani itawale siku zote.

“Wakati wote wa maadhimisho ya Kongamano la Ekaristi Takatifu,
tulibebe Taifa letu, tulibebe Kanisa letu, tuubebe ulimwenu wotena
tuyabebe matatizo yetu ili Mungu atusamehe maovu yetu ili amani
itawale siku zote” alisema

Hata hivyo alisema kila Mkristo anatakiwa kuhakikisha kile
anachokisema kinakuwa na tafsiri katika mawazo ili kuepuka kuzungumza
kitu kinachochochea mparaganyiko wa watu katika maisha.

“Hebu tujitahidi kwa kile tunachokisema lazima kiwe na tafsiri katika
mawazo yetu. Tuwe na moyo wa ibada, tusiadhimishe wakati hatuna moyo
wa upendo, tuwe wakarimu, tuwe na huruma, tuwe na faraja, tuwe wapole
pale tunapoudhiwa ili kutafuta suluhu katika amani” alisema.

Pia amewataka Wakristo kumuombea Baba Mtakatifu Benedicto XVI katika
utume wake ili aweze kufanya kazi kwa ujasiri na kukabiliana na
changamoto zinazojitokeza katika utume wake.

Kongamano la Ekaristi Takatifu kitaifa linafanyika jimboni Iringa
ambapo kilele chake kinatarajiwa kufanyika Juni 10 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment